Tuesday, 11 March 2014

WAZEE WA YOMBO KILAKALA WATOA YA MOYONI

Mhasibu wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Joyna Mwafute akimlisha  chakula mmoja wa wazee waishio katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo kilakala Bi.Tabu Juma( 65) wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipofika kituoni hapo kutoa misaada wa vyakula,mafuta ya kula,blanketi na mashuka vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5/-.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  wakiwa katika picha ya pamoja na wazee wasiojiweza wa kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation ilichopo Yombo Kilakala wakati walipokwenda kuwapa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka, blanketi,vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2.5/-.

.......................................................................................
WAZEE WALIA NA SERIKALI
 
Wazee wa Yombo Kilakala wameililia Serikali juu ya kukosa huduma stahiki kama ukosefu wa matibabu na matunzo bora kwasababu ya kunyanyapaliwa na kutelekezwa  na familia zao hivyo kuishi katika mazingira magumu.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na wazee waishio Yombo Kilakala wilayani Ilala jijini Dar es salaam  wanaofadhiliwa na Taasisi ya Tushikamane pamoja walipotembelewa  na Wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa Ajira ya Erolink  kwa lengo la kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu yenye zaidi ya shilingi milioni 2.5/-.
 
Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, Bi.Julietha Mchanga(90) alisema kuwa  changamoto kubwa nyowakabili ni  kukosa matunzo na matibabu yasiyostahili kwani wengi wao hawana msaada.
 

Bi. Mchanga alibainisha kuwa hayo yanatokana na kukimbiwa na  kutothaminiwa na watoto wao hivyo kukosa matunzo jamboa mabalo huwafanya wazee waishi maisha magumu.
 
Vilevile alisema kuwa sera ya kutunza wazee haitekelezwi ipasavyo hivyo ni wakati mwafaka kwa serikali na jamii kwa ujumla kutambua na kuwakumbuika kwani ni miongoni mwa watu waliosahaulika hapa nchini.
 
Mfanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Zabida Kibiki akimvisha shuka baada ya kumkabidhi msaada huo John Shitundu ambaye ni miongoni mwa wazee waliopo chini ya kituo chaTushikamane Pamoja Foundation wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa kituo hicho Rose Mwapachu.
Kwa upande wake, Taddious Ndyetabuula  ambaye ni Meneja mikataba wa kampuni ya Erolink Alisema kuwa  msaada walioutoa  kwa wazee hao  umekwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani lakini pia lengo kuu ni kujumuika na  wazee wasiojiweza  ili  wajione kwamba hawajasahaulika.
 
“Msaada huu wa vyakula,mafuta ya kupikia ,sabuni  na mashuka pamoja na hafla hii ya  kujumuika na wazee kwaajili ya chakula cha mchana ni endelevu ,hivyo sisi kama Erolink ni jukumu na wajibu wetu  kuhakikisha kwamba tunawasaidia na kuwathamini wazee wanaoishi katika mazingira magumu” alisisitiza Ndyetabuula.
 
Baadhi ya wazee wanaoishi na kutunzwa katika Kituo cha  Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,wakicheza pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  walipowatembelea wazee hao mahususi kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5/-.

Naye  Mwenyekiti  wa taasisi ya  Tushikamane Pamoja, Rose Mwapachu alisema kuwa  hana budi kuishukuru Kampuni ya Erolink kwa msaada walioutoa kwa wazee haoo lakini pia alitumia fursa hiyo kuyaomba mashirika na makampuni mbalimbali kuwaungamkono katika jitihada zao za kuhakikisha    ustawi wa maisha bora ya  wazee hapa nchini.
 
“Tuna utaratibu wa kutoa misaada ya kibinadamu  kwa wazee katika vituo mbalimbali jijini hapa ikiwemo kinondoni,manzese,tandale,magomeni na maeeo mengine lakini uwezo wetu ni mdogoi tunahitaji wafadhili zaidi kwaajili ya  kujenga majengo kuishi hawa wazee kwani wengine hawana makazi iantubidi kuwalipia kodi”Alisisitiza Mwapachu
 
Aliongeza kuwa hivi  sasa serikali imewapa kiwanja huko Kwembe (Nje kidogo ya jiji la Dar es salaam)na wapo katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi  lakini pi8a bado wanahitaji msaada zaidi iliwaweze  kukamilisha ujenzi huo ili waweze kuwatunza na kuwalea  wazee  katika mazingira mazuri.

Monday, 10 March 2014

ANGALIA BARABARA YA SAKOTA, TEMEKE ILIVYOBOMOKA NA KUHATARISHA WAPITAJI WA VYOMBO VYA USAFIRI

Dereva wa lori akilikwepa shimo litokanalo na kukatika kwa barabara ya Sakota wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Wakazi wa eneo hilo wamesema kwamba barabara hiyo iliharibika tangia desemba mwaka jana huku wakala wa barabara nchini(Tanroads) wakitembelea eneo hilo bila kuchukulia hatua zozote za ukarabati.
Barabara hiyo ikiwa imeharibika kwa kiasi kikubwa hivyo kuhatarisha wapitaji wa vyombo vya usafiri.

Dereva pikipiki akimuangalia dereva lori kwa kuhofia kubanwa upande wa shimo ambapo barabara ya Sakota, Temeke imeharibika.

JINSI NYAMA CHOMA FESTIVAL ILIVYOBAMBA JIJINI DAR

Hapa Mpishi akichoma Nyama kwa makini.
Wadau Amani Nkurlu(wapili kulia), Leonard Nkurlu(kulia) pamoja na wadau wengine wakipata wasaa wa ukodak kwenye Nyama Choma Festival jumamosi jijini Dar es Salaam.
Nyama ya kuku ikichomwa.
Mtangazaji wa Clouds fm, Adam Mchomvu(kushoto) pamoja na DJ K3(katikati) wakisawazisha swala la mziki kwenye Nyama Choma Festival iliyofanyika jumamosi jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakicheza na kufurahia mziki katika Nyama Choma festival iliyofanyika jumamosi viwanja vya Posta, Kijitonyama.
Maana halisi ya Tamasha la Nyama Choma. Hapa Nyama ya Mbuzi ikichomwa.
Wadau kutoka kona zote za jiji la Dar es Salaam wakifurahi na kubadilishana mawazo katika viwanja vya Posta ambapo Nyama Choma Festival ilifanyika siku ya jumamosi. Ulikuwa ni mkusanyiko wa aina yake.
Wadau

Thursday, 6 March 2014

Mwanaharakati Jane Magigita akabidhiwa tuzo ya Dk. Martin Luther King kwa kupigania haki za kisheria za wanawake

Mwanaharakati Jane Magigita(kulia) akipokea tuzo ya Dk. Martin Luther King kutoka kwa Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser.
Watu waliohudhuria tukio hilo wakiwemo Mwenyekiti Mtendaji wa IPP media, Dk. Reginald Mengi na Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhan ambao pia walishawahi kupokea tuzo hiyo awali.
 ..................................................................................................................................................
Kaimu Balozi Virginia M. Blaser, amtunukia Bi Jane Magigita-Milyango tuzo ya Dk. Martin Luther King kwa kupigania haki za kisheria za wanawake.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Virginia M. Blaser, alimtunukia Bi. Jane Magigita–Milyango tuzo ya Haki ya Dk. Martin Luther King kwa mwaka 2014 kwa kutambua jitihada zake kubwa za kutetea haki za kisheria za wanawake, hususan katika kukabiliana na tatizo la ukatili wa kijinsia na suala la urithi na matumizi ya ardhi kwa wanawake wa vijijini. Bi Magigita ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali  iitwayo Equality for Growth (EfG) iliyosajiliwa mwaka 2008.  Vile vile ni mwanzilishi na mjumbe wa bodi wa taasisi kadhaa za hapa nchini ikiwa ni pamoja na tawi la Tanzania la African Evangelical Enterprise (AEE-Tz) na Children's Dignity Forum (CDF).  Hali kadhalika Bi. Magigita ni mjumbe wa timu maalumu ya wataalamu kutoka katika taasisi zinazotoa msaada wa kisheria.

Tuzo ya Haki ya Dk. Martin Luther King, Jr. hutolewa kila mwaka na Balozi wa Marekani nchini Tanzania ili kuenzi maisha na mafanikio ya Dk. King na ya Mtanzania ambaye kama ilivyokuwa kwa Dk. King, amejitoa kwa dhati kuwahudumia na kuwapigania wengine.

Katika hotuba yake, Kaimu Balozi Blaser alimpongeza Bi. Magigita kwa maono, ujasiri na kujitoa kwake kwa dhati katika kukabiliana na vitendo vya uonevu na ukiukwaji wa haki:  “Bi Magigita anapaisha na kuzipa nguvu sauti za Watanzania wenzake ili nao waweze kudai haki zao kwa njia za amani. Katika kipindi cha miaka 13 iliyopita, Bi Magigita amekuwa akitoa huduma ya msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia moja kwa moja au kwa kupitia Vituo mbalimbali vya Msaada wa Kisheria. Kutokana na jitihada za Bi. Magigita wanawake hawa pamoja na watoto wao  wameweza kukataa uonevu unaoambatana na ukatili wa kijinsia. Kama ilivyokuwa kwa watu walioandamana na Dk. King wanawake hawa wamejenga ujasiri na uwezo wa kudai haki zao za kisheria kama raia walio chini ya sheria za taifa hili adhimu.”

Kaimu Balozi Blaser aliendelea kusema kuwa, kama ilivyokuwa kwa Dk. King, Bi Magigita haogopi kutumia mivutano iliyopo katika jamii kama fursa ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii husika.

JINSI LUPITA NYONG'O NA MWANAMUZIKI RIHANNA WALIVYOVUTA MACHO YA WATU KWENYE PARIS FASHION SHOW WEEK

 
Muigizaji kutoka Kenya, Lupita Nyong'o na Mwanamuziki wa Marekani, Rihanna wakifurahia jambo kwenye Miu Miu fashion, Paris jana.
Rihanna na Lupita wakipata wasaa wa ukodak.
Rihanna na Lupita wakiwa kwenye mstari wa mbele kabisa kwenye Miu miu fashion, Paris jana.
Lupita akijipiga ukodak 'selfie' na warembo wenzake.
Muigizaji wa Marekani, Jared Leto akiwa na Mwanamuziki Rihanna kwenye Miu miu fashion, Paris jana.
Lupita Nyong'o akiteta jambo na muigizaji wa Marekani, Jared Leto. Hivi karibuni kumekuwa na tetesi mbalimbali za waigizaji hawa kuwa na uhusiano zaidi ya urafiki.

Muigizaji kutoka Kenya, Lupita Nyong'o akiongea na muigizaji na mwanamitindo wa Marekani, Ashley Oslen.