.......................................................................................
WAZEE WALIA NA SERIKALI
Wazee wa Yombo Kilakala wameililia Serikali juu ya kukosa huduma stahiki kama ukosefu wa matibabu na matunzo bora kwasababu ya kunyanyapaliwa na kutelekezwa na familia zao hivyo kuishi katika mazingira magumu.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na wazee waishio Yombo Kilakala wilayani Ilala jijini Dar es salaam wanaofadhiliwa na Taasisi ya Tushikamane pamoja walipotembelewa
na Wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa Ajira ya Erolink kwa lengo la kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu yenye zaidi ya shilingi milioni 2.5/-.
Akizungumza kwa niaba ya wazee
wenzake, Bi.Julietha Mchanga(90) alisema kuwa changamoto kubwa nyowakabili ni kukosa matunzo na matibabu yasiyostahili kwani wengi wao hawana msaada.
Bi. Mchanga alibainisha kuwa hayo yanatokana na kukimbiwa na kutothaminiwa na watoto wao hivyo kukosa matunzo jamboa mabalo huwafanya wazee waishi maisha magumu.
Vilevile alisema kuwa sera ya kutunza wazee haitekelezwi ipasavyo hivyo ni wakati mwafaka kwa serikali na jamii
kwa ujumla kutambua na kuwakumbuika kwani ni miongoni mwa watu waliosahaulika hapa nchini.
Kwa upande wake, Taddious Ndyetabuula ambaye ni Meneja mikataba wa kampuni ya Erolink Alisema kuwa msaada walioutoa kwa wazee hao umekwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani lakini pia lengo kuu ni kujumuika na wazee wasiojiweza ili wajione kwamba hawajasahaulika.
“Msaada huu wa vyakula,mafuta ya kupikia ,sabuni na mashuka pamoja na hafla hii ya
kujumuika na wazee kwaajili ya chakula cha mchana ni endelevu ,hivyo sisi kama Erolink ni jukumu na wajibu wetu kuhakikisha kwamba tunawasaidia na kuwathamini wazee wanaoishi katika mazingira magumu” alisisitiza Ndyetabuula.
Naye Mwenyekiti wa taasisi ya Tushikamane Pamoja, Rose Mwapachu alisema kuwa hana
budi kuishukuru Kampuni ya Erolink kwa msaada walioutoa kwa wazee haoo
lakini pia alitumia fursa hiyo kuyaomba mashirika na makampuni
mbalimbali kuwaungamkono katika jitihada zao za kuhakikisha ustawi wa maisha bora ya wazee hapa
nchini.
“Tuna utaratibu wa kutoa misaada ya kibinadamu kwa wazee katika vituo mbalimbali jijini hapa ikiwemo kinondoni,manzese,tandale, magomeni na maeeo mengine lakini uwezo wetu ni mdogoi tunahitaji wafadhili zaidi kwaajili ya kujenga majengo kuishi hawa wazee kwani wengine hawana makazi iantubidi kuwalipia kodi”Alisisitiza Mwapachu
Aliongeza kuwa hivi sasa serikali imewapa kiwanja huko Kwembe (Nje kidogo ya jiji la Dar es
salaam)na wapo katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi lakini pi8a bado wanahitaji msaada zaidi iliwaweze kukamilisha ujenzi huo ili waweze kuwatunza na kuwalea wazee katika mazingira mazuri.
No comments:
Post a Comment