Friday, 3 January 2014
Shehena ya meno ya Tembo yanaswa Dar
![]() |
Meno ya Tembo |
Hata hivyo, waandishi wa habari ambao walifuatana na Kaimu Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tabu Nziku, jana kwenye Bandari hiyo ili wakashuhudie kukamatwa kwa meno hayo walizuiliwa kwa muda wa saa mbili na walinzi wa Suma JKT kwa sababu ambazo hazijajulikana.
Licha ya kujitambulisha kuwa ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, maafisa hao waliwazuia kufanya kazi yao, jambo lililozusha mjadala na mabishano kwa muda mrefu pamoja na kuwepo kwa maofisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Huku mabishano hayo yakiendelea walinzi hao walikuwa wanashinikiza waandishi wa habari watolewe nje, pamoja na kuwa wakati huo walikwishaingia ndani, na kugoma katakata kuwaonyesha kontena hilo.
Kaimu Mrugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande, alithibitisha kuwapo kwa kontena hilo lenye meno ya tembo, lakini alisema yeye hana uwezo wa kulizungumzia suala hilo bali wenye mamlaka hiyo ni Naibu Waziri pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara.
Aliongeza kuwa kwa sasa anafanya mawasiliano na ngazi hizo za juu na atakapokuwa tayari atamjulisha Afisa Habari ili awaite waandishi kwa ajili ya kulizumgumzia suala hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu, alisema amezipata taarifa hizo, lakini kwa muda huo alikuwa njiani akitokea Maswa na kwamba wizara inaandaa taarifa rasmi ili kulizungumzia jambo hilo ambayo itasambazwa kwenye vyombo vya habari.
Hata NIPASHE ilipomtafuta Kamanada wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, simu yake ya mkononi ilipokelewa na msaidizi wake ambaye alisema kuwa Kamishna Kova alikuwa katika kikao.
Matukio ya kuuawa kwa tembo yamekithiri nchini na hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa sensa ya ndovu katika Pori la Hifadhi ya Selous imekamilika, lakini taarifa yake inatisha kwani kuna ndovu 13,084 tu wakati mwaka 1976 walikuwepo tembo 109,419.
Aliongeza kuwa watu 1,030 walikamatwa pamoja na silaha za kijeshi 18, za kiraia 1579, na shehena kubwa za meno ya tembo na nyara nyingine navyo vilikamatwa, na watu kadhaa wameshafikishwa mahakamani na kwamba awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza Ujangili itaanza.
CHANZO:
NIPASHE
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa kuwasili kesho.
Mwili
wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, unatarajiwa kuwasili
Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kutokea Afrika Kusini kesho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi hayo kitaifa, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Alisema mwili wa marehemu utawasili na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini wakati wa mchana na kupelekwa moja kwa moja nyumbani kwake Mikocheni B na baadaye jioni utapelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Jumapili saa nne na nusu asubuhi mwili huo utapelekwa nyumbani kwake na baadaye utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee, kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho.
“Wananchi wote watakaoshindwa kusafiri kwenda Iringa watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho katika ukumbi wa Karimjee, hivyo wananchi mnaombwa kufika eneo hilo,” alisema Lukuvi.
Alisema alasiri mwili wa marehemu utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kwa safari ya kuelekea mkoani Iringa.
Lukuvi alisema kuwa majira ya saa 10 alasiri mwili utawasili Uwanja wa Ndege wa Iringa baadaye kuagwa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo mkoani humo.
Alisema Jumapili saa 11:30 jioni mwili wa marehemu Mgimwa utasafirishwa kuelekea kijijini kwake Magunga, na Jumatatu mchana shughuli za mazishi zitafanyika katika kijiji hicho.
Alifafanua kuwa serikali imeunda kamati kwa ajili ya kushughulikia msiba huo kuanzia kuwasili kwa mwili uwanja wa ndege hadi siku ya mazishi kijijini kwake.
Alisema kamati hiyo inayoongozwa na yeye, ikiwa na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Afya, Bunge, Ikulu, na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Alisema mbali na kuwapo kwa kamati hiyo, pia kumeundwa kamati nyingine ndogo ya mkoa wa Iringa inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma.
“Hivyo kwa wakazi wa Iringa, marafiki zake na jamaa wa karibu watapata nafasi ya kuuaga mwili wa marehemu katika ukumbi huo, shughuli zitakazoongozwa na kamati ndogo ya Iringa,” alisema Lukuvi.
Lukuvi alisema kuhusu sababu iliyosababisha kifo cha marehemu Mgimwa itaelezwa siku ya kuuaga mwili katika ukumbi wa Karimjee.
“Hatuwezi kuficha sababu ya kifo chake, hata hivyo, mwili ukifika uwanja wa ndege utakuja na death certificate (hati ya kifo), hivyo kuweni na subira na muweke akiba ya habari,” alisema Lukuvi.
JIMBONI KALENGA WAMLILIA
Wakati huo huo, wakazi wa Jimbo la Kalenga, wilaya ya Iringa vijijini, mkoani Iringa, wamesema kifo cha mbunge wao, Waziri, Dk. Mgimwa, kimeacha pengo kubwa kwa kuwa aliwathamini na kutatua matatizo yao kwa wakati.
Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti, Raphael Lengesia, alisema baada ya kusikia taarifa ya kuhusu kifo cha mbunge wao alipata mshtuko kwa kuwa ni pengo ambalo halitazibika kwao.
“Sisi kama wakazi wa jimbo hili, tumesikitika sana kupata taarifa hizi ambazo zimemgusa kila mmoja wetu kutokana pengo hili ambalo ametuachia, tulikuwa tukiuthamini mchango wake katika kutusaidia kutatua matatizo yetu wakati akiwa jimboni,” alisema Lengesia.
Maimuna Nzigiwa, mkazi wa Ifunda, alisema mbali na kuwa na majukumu ya kitaifa, Dk. Mgimwa aliwatumikia wapiga kura wake kwa uaminifu na bidii kubwa.
“Hatuna hakika kama tutapata kiongozi mwenye busara kututetea wananchi hasa wa vijijini kulingana mambo mengi aliyoyafanya hapa kijijini kwetu,” alisema Nzigiwa.
Aliongeza kuwa, marehemu alikuwa akiwapigania kwenye masuala mbalimbali ikiwamo barabara, shule, zahanati hususan maji na kuwawezesha kupata maji na kwamba wataendelea kumkumbuka.
Ramadhan Salehe, alisema mchango wa Dk. Mgimwa ulikuwa mkubwa na kuwataka viongozi wengine kuiga ili kuwa na maendeleo endelevu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa, Steven Mhapa, alisema ni pigo kubwa kutokana na mchango wa marehemu katika kuisaidia jamii na kuwa imepoteza mtu mwenye busara na mchapakazi, ambaye alishirikiana na halmashauri hiyo katika kuwatafutia wafadhili kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo.
MTOTO WAKE AZUNGUMZA
Akizungumza na NIPASHE, nyumbani kwao Mikocheni B jana, mtoto wa marehemu, Godfrey Mgimwa, alisema baba yake enzi za uhai wake alikuwa ni mtu wa dini na kwa jinsi hiyo aliwalea katika misingi ya maadili ya kidini, na kwa kifo chake wamempoteza mzazi aliyekuwa wa umuhimu sana kwao.
Alisema, baba yake pia hakuwa mtu mbinafsi kwani aliwasaidia watu wengi wakiwamo wa jimboni kwake.
Kuhusu idadi ya watoto, Godfrey alisema, baba yake amemwacha mama yake ambaye amekuwa akimuuguza nchini Afrika Kusini, watoto wa kike wawili na wa kiume kadhaa, kwani idadi kamili ya watoto alioacha marehermu baba yake ni siri yao.
Kwa mujibu wa Godfrey, baba yake alikuwa mtu aliyependa familia yake, kwani hakuwa mwepesi kuwapa mali ovyo bila sababu za msingi hata kama alikuwa ni mtu mwenye nafasi kubwa serikalini.
Baadhi ya viongozi wa serikali ambao hadi jana walikuwa wamefika nyumbani hapo kwa ajili ya kutoa pole, ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi; Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.
Wengine ni manaibu mawaziri wa Fedha, Janet Mbene na Saada Mkuya; Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa.
Imeandikwa na Gwamaka Alipipi, Isaya Kisimbilu, Dar na George Tarimo, Iringa.

Wednesday, 1 January 2014
JINSI MAPOKEZI YA MWAKA MPYA YALIVYOBAMBA JIJINI DAR
Sehemu ya kundi la watu waliofurika eneo la Slipway wakijumuika na familia na marafiki zao kwa ajili ya kusherekea mwaka mpya. |
Vijana wakifurahia mwaka mpya kwa shangwe na kupiga vuvuzela eneo la Slipway. |
Watoto nao hawakucheza mbali na sherehe za mwaka mpya. |
Raia wa kigeni wakisherekea mwaka mpya kwa kujumuika na watanzania enea la Slipway, water front. |
Marafiki wakigonga chiazz kama ishara ya kuupokea mwaka mpya. |
Wadau mbali mbali waliokwepo Slipway, waterfront kusherekea. |
Warembo nao hawakusita kuwa na nyuso za furaha mara baada ya mwaka mpya kuwadia. |
![]() |
Namimi nikapose na warembo kutoa tabasamu la mwaka 2014. |
Tabasamu la mwaka mpya eneo la Masaki. |
![]() |
Watu wakibadilishana mawazo na kupanga mipango ya mwaka mpya. |
Wadau. |
Mdau Bambo Magingo pamoja na dada yake. |
BREAKING NEWS:WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA
RAIS KIKWETE ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea
kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa
William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa Jimbo la Kalenga (Mkoa wa Iringa)
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais
Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa
linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia
nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.
Kifo
cha Mheshimiwa Mgimwa kimetangazwa mchana wa leo, Jumatano, Januari Mosi, 2014,
na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika
tangazo lake, Balozi Sefue amesema kuwa Waziri Mgimwa ameaga dunia asubuhi ya
leo saa 5:20 (Saa za Afrika ya Kati) katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic ,
Pretoria, Afrika Kusini ambako amekuwa amelazwa kwa muda sasa.
Balozi
Sefue amesema kuwa maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Waziri Mgimwa
yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia yake na kuwa taarifa zaidi
kuliko suala hilo zitatolewa baadaye kwa kadri zinavyopatikana na maandalizi
yanavyoendelea.
Katika
salamu zake kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na kwa familia ya Marehemu
Mgimwa, Rais Kikwete amesema: “Sina
maneno ya kutosha kuelezea mshtuko na huzuni yangu kubwa kufuatia taarifa za
kifo cha Mheshimiwa Mgimwa. Binafsi nimemtembelea mara mbili kwenye Hospitali
alikokuwa amelazwa na mara ya mwisho hali yake ilikuwa imeimarika. Tulizungumza
kwa kiasi cha dakika 10 hivi akanielezea nia yake na tamaa yake ya kurejea nyumbani
kwa sababu hali yake ilikuwa nzuri.”
Ameongeza
Mheshimiwa Rais Kikwete: “Sote tunajua mchango wake katika Serikali. Sote
tulitamani kuendelea kuwa naye, lakini haya ni mapenzi ya Mungu.”
“Napenda
kutoa pole nyingi na rambirambi zangu za dhati kwa wana-familia wote kwa
kuondokewa na mhimili wao. Naungana nanyi katika kuomboleza msiba huo mkubwa.
Napenda mjue kuwa msiba huu ni msiba wangu pia. Machungu yenu ni majonzi yangu,”
amesema Rais Kikwete.
Rais
pia amewatumia rambirambi wananchi wa Jimbo la Kalenga akisema kuwa wamempoteza
mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi yao.
Subscribe to:
Posts (Atom)