Saturday 22 February 2014

TIMU YA KIKAPU YA OUTSIDERS YACHAPWA NA TIMU YA MBC(MBEZI BEACH BBALL CLUB) VIKAPU 76 KWA 68 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI JANA

Mchezaji wa timu ya Outsiders(kushoto) akiangalia jinsi ya kuwafungulia njia  wachezaji wenzake kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya MBC jana viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Timu ya MBC ilishinda vikapu 76-68 ambapo hadi robo yapili timu ya Outsiders ilikuwa inaongoza.

Wachezaji wa timu ya Outsiders na MBC wakijiweka teyari kuugombania mpira uliorushwa na mchezaji wa Outsider, Big(6).
Mchezaji wa timu ya Outsiders, Dady(9) akizuia lango dhidi ya mchezaji wa timu ya MBC, Bato katika mechi ya kirafiki iliyochezwa jana viwanja vya Chuo kikuu cha Dar  es Salaam. 
Mchezaji wa timu ya MBC, Joseph Kisusi(23) akichoma dhidi ya wachezaji wa timu ya Outsiders jana viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Timu ya MBC iliishinda timu ya Outsiders kwa vikapu 76-68.
Wachezaji wa timu ya MBC(kulia na kushoto) wakimuangalia mchezaji wa timu ya Outsiders(katikati) akirusha mpira kwenye kikapu.
Wachezaji wa timu ya Outsiders wakiangalia mpira ukiingia kwenye kikapu mara baada ya mchezaji wa MBC kuurusha.
 
Mchezaji wa timu ya MBC, Cornelly(kulia) akirusha mpira kwenye kikapu huku akizuiwa na mchezaji wa timu ya Outsiders.
Wachezaji wa timu ya Outsiders wakijadili jambo kipindi cha mapumziko.

No comments:

Post a Comment