Thursday 30 January 2014

Mwanafunzi wa Ardhi atoa changamoto kwa vijana kupitia kitabu chake cha 'Safari Ya Ndoto'

 
Mtunzi wa kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' Bw. Aman Nguku (kulia) ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo cha Ardhi akiwaelezea waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) kuhusu kitabu hicho alichokizindua jana jijini Dar es Salaam. (Picha Zote na Atuza Nkurlu)
Nguku anaelezea kwamba kitabu hicho yenye kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi,” inatoa hamasa kwa watu hasa hasa kundi la vijana waweze kuwa na uthubutu wa kutimiza malengo yao katika maisha. Wanaoshuhudia ni mama yake mkubwa Bi. Anna Kikwa na baba yake mdogo Bw. Emmanuel Mallewo.
Bi. Kikwa (kushoto) na Bw. Mallewo wakionyesha kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' alichokiandika mwanao Aman (katikati) anayesoma shahada ya uchumi mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Ardhi.
Mtunzi wa kitabu cha 'Safari Ya Ndoto' Aman Nguku akihojiwa na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kitabu hicho jana. Wanaoshuhudia ni walezi wake Bi. Kikwa na Bw. Mallewo.
.............................................................................................
 
Vijana wakitanzania wameaswa kuacha kulalamika na kuishi katika maisha ya nadharia, badala yake wameshauriwa kubadilika kuwa watendaji na wenye uthubutu wa kutimiza malengo yao katika maisha.
 
Maneno hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Amajat Investment Bw. Aman Nguku  jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa kitabu chake kiitwacho ‘Safari Ya Ndoto’ inayobeba kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi.”
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Nguku alisema imefika wakati sasa watanzania hasahasa kundi la vijana waamke kutoka usingizini na kutimiza malengo yao ya kimaisha ambayo wanapenda kufikia.
 
“Imetosha kusema kesho, kufikiri bila kutenda na kuongea bila vitendo. Kinachotakiwa ni kuanza utekelezaji,” alinukuu Bw. Nguku kutoka kwenye kitabu chake chenye kurasa 108.

Akielezea madhumuni ya kuandika kitabu hicho, Bw. Nguku ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam alisema:

“Hiki kitabu ni mahususi kwa wale watu ambao wana ndoto mbali mbali katika maisha yao lakini hawajui pakuanzia, iwe ndoto ya kuwa mfanyabiashara maarufu, mwanasiasa au daktari bingwa. Hiki kitabu ni ramani maalum kwao.”

Aliendelea, “Kitabu hiki kinaweza pia kuwa changamoto kwa wale ambao wamekata tamaa katika maisha. Kwa kusoma maandishi ya kitabu hiki, wanaweza wakafufua ndoto zao na kufanikiwa katika yale waliyoyapanga.”

‘Safari Ya Ndoto’ pia inabeba dondoo kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, mfanyabiashara maarufu Bw. Reginald Mengi na Mkurugenzi Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Bw. Patrick Ngowi.
 
Kitabu hiki kinasambazwa katika maduka mbali mbali jijini Dar es Salaam na nchi nzima ili watanzania wengi wapate kukisoma. Kinauzwa kwa Tsh 5000 tu.
Kwa sasa, mtunzi Nguku pia anaandika vitabu vingine viwili venye vichwa ‘Ndogo lakini muhimu, kesho’ na ‘What is life for!(Maisha ni ya nini!).

Sunday 19 January 2014

BREAKING NYUUZZ: UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI ULIOFANYWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE

            Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-

 
                1.0 OFISI YA RAIS
                  Hakuna mabadiliko.
 

                2.0  OFISI YA MAKAMU WA RAIS
             
             2.1  Waziri wa Nchi (Muungano) - Hakuna mabadiliko
             2.2   Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE
                        Waziri wa Nchi (Mazingira).

               2.3    Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
                    Naibu Waziri  
                                                               

           3.0 OFISI YA WAZIRI MKUU
                 Hakuna mabadiliko
 

           4.0 WIZARA
           4.1  WIZARA YA FEDHA
            
             4.1.1 Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)
                      Waziri wa Fedha
                  Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)           
                  Naibu Waziri wa Fedha

             4.1.2 Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
                  Naibu Waziri wa Fedha

           4.2  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
                Hakuna mabadiliko
 
         4.3 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
      
         4.3.1 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
                 Waziri wa Katiba na Sheria

           4.3.2 Naibu Waziri - Hakuna mabadiliko
 
         
           4.4   WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
                Hakuna mabadiliko

 
         4.5   WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
         4.5.1 Waziri - Hakuna mabadiliko
 
         4.5.2    Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
                     Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
 
         4.6       WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
                     Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
                     Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
 
           4.7        WIZARA YA UJENZI
                    Hakuna mabadiliko
 

          4.8       WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
          4.8.1    Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
                      Waziri wa Mambo ya Ndani                        
 
             4.8.2        Naibu Waziri - Hakuna Mabadiliko


         4.9      WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
           4.9.1     Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
                    Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
         4.9.2     Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
                    Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

 
         4.10   WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
         4.10.1 Waziri:  Hakuna mabadiliko

         4.10.2  Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
                      Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

          14.11 WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
          14.11.1  Waziri: Hakuna mabadiliko

          14. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
                       Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

         
          14.12  WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

          14.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
                       Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

             14.12.2 Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)
                      Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
 

 

14.13      WIZARA YA KAZI NA AJIRA
                      Hakuna mabadiliko
                                                              
           14.14      WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
                     Hakuna mabadiliko
14.15   WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

          14.15.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
 
         14.15.2  Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
                      Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
 
         14.16   WIZARA YA MAJI
         14.16.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
         14.16.2  Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
                      Naibu Waziri wa Maji

  
       14.17  WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
                 14.17.1  Waziri - Hakuna mabadiliko

        14.17.2   Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
                  Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

        4.18     WIZARA YA UCHUKUZI
                   Hakuna mabadiliko
 
         4.19     WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
                 
         4.19.1  Waziri -  Hakuna mabadiliko

         4.19.2  Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
                    Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

            4.20     WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
         4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
                   Waziri wa Maliasili na Utalii

         4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
                    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
 
           4.21     WIZARA YA NISHATI NA MADINI
         4.21.1    Waziri - Hakuna mabadiliko

           4.21.2    Naibu Waziri (Madini) - Hakuna mabadiliko
         4.21.3  Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)                                 
                     Naibu Waziri (Nishati)





Balozi Ombeni Y. Sefue

KATIBU MKUU KIONGOZI

Ikulu
DAR ES SALAAM
19 Januari, 2014  


Saturday 18 January 2014

MNYIKA KUKUTANA NA WANANCHI WA PEMBEZONI YA BARABARA YA MOROGORO KESHO (19 JANUARI 2014)

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ubungo inatoa taarifa kwa umma kwamba John Mnyika (Mb) jumapili tarehe 19 Januari 2014 atakutana na wananchi wenye makazi pembezoni mwa Barabara ya Morogoro wanaothirika na nyongeza ya hifadhi kinyume cha sheria ya ardhi na amri ya Mahakama Kuu.

Mkutano huo wa Mbunge na wananchi utafanyika katika eneo la Luguruni Makondeko na utahusisha pia kamati ya waathirika wa hifadhi ya barabara pamoja na wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali ya majimbo ya Ubungo, Kisarawe na Kibaha.

Wananchi hao wamekuwa na malalamiko ya haki zao za msingi za makazi na za kibinadamu kuvunjwa kwa maagizo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli ambayo hutekelezwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) kinyume na sharia.
 
Aidha, kwa nyakati mbalimbali katika ya mwaka 2011, 2012 na 2013 yamejitokeza malumbano ndani na nje ya Bunge baina ya Mbunge Mnyika (akiwakilisha wananchi) na Waziri Magufuli (akisisitiza msimamo wa serikali) kuhusu utata wa upana wa barabara ya Morogoro na haki za wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni ya barabara hiyo.
Kwa upande mwingine, Malalamiko hayo ya wananchi yalishawahi kufikishwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia shauri Na 80 la 2005 na hukumu kutolewa tarehe 31 Mei 2013, ambapo Mahakama Kuu ilitamka kuwa sheria ya The Highway Ordinance Cap 167 Government Notice No 161 of 5/5/1967 ambayo hutumiwa na Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuingia katika ardhi  za wananchi “ni batili kwa kutofautiana na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”.

Kamati ya waathirika wa hifadhi ya barabara imemwandikia barua mbunge kumweleza kuwa mahakama kuu imeamua kuwa  inayodaiwa na walalamikiwa (Wizara ya Ujenzi) kuwa ni hifadhi ya barabara (hadi Mita 121 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro pande zote mbili), iligawiwa kwa walalamikaji kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi wakati wa operesheni vijiji ya miaka 1970, na hivyo kwa mujibu wa vifungu vilivyotajwa hapo juu  ni mali halali ya wananchi.

Katika mkutano huo, mbunge atasikiliza malalamiko ya wananchi juu ya hatua ya Wizara ya Ujenzi na Tanroads bila kujali hukumu ya mahakama kuendelea kushikilia ardhi za wananchi zilizo nje ya mita 30 kutoka katikati ya barabara isivyo halali bila ya kulipa fidia stahili katika maeneo ambayo Serikali inataka kuyatwaa kwa ajili ya miundombinu na kuwazuia wananchi kuendeleza maeneo yao yaliyo nje ya mipango ya maendeleo ya umma.

Mbunge anakwenda kukutana na wananchi kwa kuzingatia kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria ya barabara namba 13 ya 2007, na Kanuni zake kupitishwa kupitia Tangazo la Serikali namba 21 la tar 23 Januari 2009. Kifungu cha 29, kinataja upana wa hifadhi za barabara kuu na za mikoa (Trunk and regional roads) utakuwa ni mita 60 tu, ikihusisha mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara”.
Aidha kifungu 27 A cha Kanuni hizo kinataja upana wa njia za barabara za lami (lanes), kwa barabara kuu (Trunk roads), kuwa hautakiwi kupungua Mita 3.25. Kwa maana hiyo hifadhi ya barabara ya mita 60 inaweza kutumika kujenga njia zinazohitajika. 
 
Maana yake ni kwamba  Wizara ya Ujenzi na Tanroads wanaweza kuheshimu maamuzi ya mahakama na sheria za nchi na kuwezesha barabara ya Morogoro kujengwa na kupanuliwa kwa njia za kutosha huku ikiacha eneo la ziada kwa ajili ya wananchi kuweza kujiendeleza na kuendeleza Jiji.

Hivyo, mkutano huo wa mbunge na wananchi utatoa nafasi ya hatua kupendekezwa zitakazowezesha kulindwa kwa haki za msingi za wananchi lakini pia kufanikisha maendeleo ya nchi kwenye sekta muhimu za ujenzi wa makazi na miundombinu.

Imetolewa tarehe 18 Januari 2014 na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo:
Aziz Himbuka
Katibu Msaidizi

HIVI NDIVYO VODACOM ILIVYOZIKU​TANISHA TIMU ZA WABUNGE WA ZANZIBAR,M​UUNGANO NA UGANDA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

Kikosi cha Timu ya soka ya Wabunge wa Bunge la Tanzania kikiwa na kombe muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuifunga timu ya Baraza la Wawakilishi bao moja kwa bila kwenye mechi maalum ya kusherehekea mika 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulidhaminiwa na kampuni ya Vodacom.
Kikosi cha Timu ya Netiboli kinachoundwa na Wabunge wa Bunge la Uganda kikiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kushuka uwanjani kuvaana na kombaini ya Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katikati  ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Hassan Saleh akimkabidhi Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho kombe lililotolewa na Vodacom kwa ajili ya mshindi wa mechi maalum kati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa Bunge la Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar na kufadhiliwa na Vodacom Tanzania.
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Pandu Ameir Kificho akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Soka ya Wabunge wa Bunge la Tanzania Amos Makala amabe pia ni Naibu Waziri wa Habari,Vijana Utamduni na Michezo kombe kufuatia kuichapa timu ya Baraza la Wawakilishi kwenye mechi maalum ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katikati ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usamabazaji wa Vodacom Hassan Saleh waliodhamini mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.
Wachezaji wa timu ya soka ya Wabunge wakipita jukwaa kuu kusalimiana na viongozi mara baada ya kumalizika kwa mechi yao na Wajumbe wa Baraza La Wawakilishi uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wabunge wa Muungano walishinda bao moja kwa bila kwenye mechi hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya Vodacom.
 
 
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usamabazaji wa Vodacom Hassan Saleh akimpongeza mchezaji wa timu ya Wabunge wa Bunge la Tanzania, Adam Malima ambae pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika mara baada ya kumalizka kwa mechi yao dhidi ya Wajumbe wa Baraza La Wawakilishi kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar. Mechi hiyo ilidhaminiwa na Kampuni ya Vodacom.

TIGO YAZINDUA MASHINE YA PILI YA "TIGOMATIC" YENYE UWEZO KAMA WA ATM

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mashine maalum ya pili ya 'TigoMatic' inayopatikana Masaki jijini Dar es Salaam mapema leo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaem Khan.
 
Meneja wa Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Henry Mboya akimuonyesha Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi jinsi mashine ya TigoMatic inavyoweza kufanya kazi katika kununua muda wa maongezi, kutuma na kupokea pesa, kulipia bili za huduma mbali mbali na kupata laini mpya ya simu.
 
 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi akitoa hotuba yake. Mstahiki Meya huyo aliipongeza Tigo kufanikiwa kuwa kampuni ya simu ya kwanza nchini Tanzania kuanzisha huduma hiyo za mashine maalum za TigoMatic.
Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaem Khan akimshukuru Mstahiki Meya, waandishi wa habari na wegeni wengine waalikwa kwa kufika katika uzinduzi huo. Mashine ya TigoMatic itakuwa wazi kwa masaa ishirini na nne kila siku.


Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi akionyesha kadi ya kipaumbele ya Tigo ambayo inatolewa kwa wateja waliokaa na Tigo kwa muda mrefu. Kadi hiyo inawezesha wateja kupatiwa huduma mbali mbali bila kupanga foleni na kuondokana na usumbufu wa gharama ndogo ndogo pindi watakapofika katika matawi yeyote ya Tigo kuhudumiwa.
......................................................................................................................................................
Tigo Tanzania imezindua mashine maalum ya pili ya TigoMatic inayowawezesha wateja wake kulipia bili za huduma mbali mbali na kuongeza salio itakayofanya kazi kwa masaa ishirini na nne kwa siku.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, ambaye ameipongeza Tigo kwa kuwa kampuni ya mawasiliano kwanza nchini Tanzania kuanzisha huduma ya aina hiyo nchini.

“Ubunifu huu wa Tigo si tu wa manufaa kwa wateja wake bali pia ni hatua mojawapo kubwa ya kimaendeleo kwa nchi yetu katika matumizi ya teknolojia za mawasiliano za kisasa duniani katika sekta ya mawasiliano,” alisema Dk Masaburi. 

Dk Masaburi alisema huduma mbalimbali zitolewazo na makampuni ya simu zikiwemo kupiga simu, SMS, intaneti pamoja na huduma za kutuma na kupokea fedha zimeleta mageuzi chnaya katika ufanyaji biashara na kuchangia kuboresha maisha ya mamilioni ya watanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika tawi la huduma kwa wateja la Tigo lililopo Masaki, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaeem Khan, amesema uzinduzi wa ‘TigoMatic’ utawawezesha wateja wa Masaki kupata huduma za zitolewazo na Tigo kwa masaa ishirini na nne kwa siku.

“Habari njema kwa watu wa Masaki ni kwamba hakutakuwa na ulazima tena kwa wateja kukaa kwenye foleni kwa ajili ya kupata huduma kutoka kwenye matawi yetu na sehemu nyinginezo za mauzo kwa sababu mashine hii ya TigoMatic inatoa msaada wa mteja kujihudumia mwenyewe,” alisema Bw. Khan.

Hii ni mashine ya TigoMatic ya pili kuzinduliwa jijini Dar es Salaam na kampuni ya simu Tigo. Mwezi uliopita Tigo ilikuwa kampuni ya simu ya kwanza nchini kuzindua matumizi ya aina hii ya mashine ilipoanza kutoa huduma hii katika tawi la makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Kijitonyama.

Akielezea jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi, Bw. Khan alisema TigoMatic ni mashine ambazo mteja anaweza akajihudumia yeye mwenyewe kama ilivyo kwa mashine za kibenki za ATM ambapo mteja anaweza akafanya miamala tofauti tofauti bila kuhitaji kuhudumiwa na mfanyakazi wa benki. Alisema kwamba wateja wa Tigo hawatakuwa na ulazima wa kujisajili upya kwa ajili ya kutumia mashine hizo.

Khan alisema kampuni inaazimia kuweka mashine zake katika matawi yake yote ya huduma kwa wateja nchi nzima pamoja na sehemu za mikusanyiko mikubwa ya watu kama vile maduka makubwa, stendi za mabasi, mitaani, viwanja vya michezo na mahospitalini.