Monday 24 February 2014

MOYES athibithsha wachezaji Phil Jones na Jonny Evans kukosa mechi ya UEFA kesho

Kocha Mkuu wa Manchester United, David Moyes(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jioni jijini Athens ambapo timu hiyo inatarajia kucheza mechi na Olympiacos katika ligi ya Mabingwa kesho.
...............................................................................................



Jonny Evans













Wachezaji wa Manchester United, Phil Jones na Jonny Evans hawajasafiri kuelekea Ugiriki kucheza ligi ya Mabingwa(UEFA Champions league) raundi ya 16 dhidi ya timu ya Olympiacos.



Phil Jones
Mabeki hao wawili wamekosa mechi kadhaa baada ya kuumia kwenye mechi waliyocheza na Stoke City, February 1 ambapo United walitoka sare ya 2-2. Jones alipata jeraha la kichwa baada ya kugongana na Jonathana Walters wakati Evans aliumia misuli ya nyuma ya goti.
Katika mkutano na waandishi wa habari leo jioni jijini Athens, David Moyes alithibitisa kukosekana kwa wachezaji hao wawili na kueleza jinsi anavyotarajia kukumbana na timu ya kigiriki, Olympiacos katika kiwanja cha Karaiskakis.
“Jones na Evans hawajasafiri nasi,  wachezaji wengine wote tupo nao,” alisema Moyes kwa waandishi wa habari. “Nilipata bahati ya kuangalia mechi ya Arsenal na Bayern Munich na kufurahia ligi ya Mabingwa."

Akizungumza kuhusiana na ligi hiyo Moyes alisema, “Kupata nafasi ya kuingia ilikuwa ni kitu muhimu cha kwanza. Kushinda kwenye kundi ni nyongeza. Natarajia hilo. Ni kweli ni mchezo mgumu, Olympiacos wanarekodi nzuri hapa, na tunafahamu, katika rekodi yetu tunasare hivyo tunabidi tucheze vizuri ili tuweze kufuzu.” Aliongezea Moyes.
Kocha huyo wa Manchester United pia alisema Olympiacos walifanya vizuri dhidi ya PSG na Benfica ambapo walitoka kwenye kundi gumu sana. Alisema wanafahamu kuwa utakuwa ni usiku mgumu sana dhidi ya Olympiacos kwasababu wanamsaada mkubwa kwani wapo nyumbani hivyo mechi hiyo haitakuwa rahisi.

No comments:

Post a Comment