Monday 24 February 2014

Ali Choki atinga ukumbini na Ambulance kwenye uzinduzi wa albamu mpya ya “Mtenda Akitendewa” ya bendi yake.

Gari la kubebea wagonjwa “Ambulance” likiingia katika ukumbi wa Dar Live likiwa limembeba Ali Choki, wakati akiingia kufanya Uzinduzi wa Albamu mpya ya bendi yake ya Extra Bongo iliyopewa jina la “Mtenda Akitendewa”.
Wasanii wa Muziki wa Dansi, Ali Choki na Banza Stone, wakiimba kwa pamoja wakati wa Uzinduzi wa Albamu mpya ya bendi yao ya Extra Bongo ya “Mtenda akitendewa”, Uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Msanii wa Muziki wa Dansi, Ali Choki akiimba mbele ya Mashabiki waliojitokeza katika uwanja wa taifa wa Burudani Dar Live, wakati wa Uzinduzi wa albamu yake mpya ya “Mtenda akitendewa” Uzinduzi huo ulidhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakitoa burudani kwa Mashabiki wa Muziki wa dansi wakati wa Uzinduzi wa Albamu mpya ya bendi ya Extra Bongo katika ukumbi wa Dar Live mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Mpiga tumba wa bendi ya Mashujaa akionyesha Ufundi katika kupiga ngoma wakati wa uzinduzi wa bendi ya Extra Bongo, “Mtenda akitendewa”.
 
Wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo “Wazee wa kizigo” wakitoa burudani kwa Mashabiki wa Muziki wa dansi wakati wa Uzinduzi wa Albamu yao mpya ya “Mtenda akitendewa” katika ukumbi wa Dar Live mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya, Linah Sanga na Amini MwinyiMkuu wakiimba kwa pamoja wimbo wa “Mtima wangu” kwa Mashabiki waliojitokeza katika Ukumbi wa Dar Live, Wakati wa Uzinduzi wa Albam mpya ya bendi ya Extra Bongo “wazee wa kizigo”, mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo pia ulisindikizwa na Bendi ya Mashujaa ulidhaminiwa na Vodacom.
............................................................................................................................................
Dar es Salaam, Februari 24, 2014 … Ilikuwa ni siku ya aina yake kwa bendi ya Extra Bongo "wazee wa kizigo" walipokuwa wakizindua albamu yao ya mtenda akitendewa na kuacha gumzo kwa mamia ya mashabiki waliojitokeza ukumbini humo asante kwa udhamini wa Vodacom kufanikisha Tamasha hilo.
Palikuwa hapatoshi katika ukumbi huo wa taifa wa burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo bendi kaadhaa za muziki wa dansi na wasanii wa bongo flava zilitumbuiza kabla ya uzinduzi wenyewe kufanyika.
Kivutio kikubwa zaidi kilikuwa ni pale ambapo kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Kamarade Ali Choki alipoingia na gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ukumbini kutumbuiza mashabiki wake waliofurika kwa wingi.
Uzinduzi wa albamu hiyo iliyokwenda kwa jina la Mtenda akitendewa ulikwenda sambamba na burudani lukuki kutoka kwa wanamuziki mbali mbali mashuhuri nchini kama vile malikia wa mipasho nchini Khadija Omari Kopa, Banza Stone, Abdul Misambano, Mashujaa Band pamoja na wasanii wa bongo flava Linah na Amini ulidhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom.
Wanenguaji wa Extra Bongo walifanikiwa vilivyo kuzikonga nyoyo za mashabiki ukumbini hapo kwa kupagawisho vilivyo jukwaani kwa staili mbali mbali mpya za uchezaji.
Kwa upande wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wa bongo flava, Linah na Amini walidhibitisha kwa nini wao ni waimbaji bora na wataendelea kuwa hivyo kwa kuonyesha kipaji cha hali ya juu katika kulimiliki jukwaa ambapo waliimba kibao chao kitamu cha ‘Omotima wange ni wewe’.


No comments:

Post a Comment