Wednesday 26 February 2014

BOMOA BOMOA JIJINI DODOMA YAWAGUSA NA WAFANYABIASHARA WA NJE YA BUNGE

Wafanyabiashara wa nje ya eneo la Bunge, Dodoma wakiwa wamesitisha biashara zao mara baada ya vibanda walivyokuwa wakiendeshea biashara vilivyokuwa vimejengwa nje ya eneo la Bunge kuvunjwa na mamlaka ya ustawishaji makao makuu(CDA) jana kwa madai kuwa vimejengwa bila kufwata taratibu za mamlaka hiyo.
  Wafanyabiashara wakiondoa mabaki ya vibanda vilivyokuwa vimejengwa nje ya eneo la Bunge, Dodoma  baada ya kuvunjiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) jana kwa madai kuwa imejengwa bila kufuata taratibu za mamlaka hiyo.
Wananchi wa Dodoma wakiangalia nyumba iliyoko Mtaa wa Oneway katika manispaa ya Dodoma baada  ya kuvunjwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) kwa madai kuwa imejengwa bila kufuata taratibu za Mamlaka hiyo.

No comments:

Post a Comment