Tuesday 31 December 2013

Wateja wa Tigo wajishindia Shilingi Milioni 160 msimu wa Mwaka Mpya


Mratibu wa promosheni za Tigo Pesa, Mary Rutta akipiga simu kupata washindi watano wa shilingi milioni 10 katika droo ya pili ya promo ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ jana. Wengine 20 walijishindia milioni 20 kila mmoja na wengine 350 walijishindia laki 2 kila mmoja iliyofanya jumla ya shilingi milioni 160 kuzolewa. Katikati ni Meneja bidhaa wa Tigo, Husni Seif na msimamizi kutoka bodi ya michezo Tanzania, Humudi Abdulhussein.                   



JUMLA ya fedha taslimu shilingi milioni 160 zimezolewa na wateja wa Tigo mara baada ya kampuni hiyo ya simu kuchezesha droo yake ya pili katika promosheni yake ya ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa droo hiyo Mratibu wa promosheni za Tigo Pesa, Bi. Mary Rutta alisema kwamba wateja watano walijishindia milioni 10 kila mmoja, wateja wengine 20 wamejishindia shilingi milioni 20 kila mmoja na wengine 350 walijishindia shilingi laki mbili mbili.

Washindi wa tano wa zawadi nono ya shilingi milioni 10 ni  Bi. Irene Francis Mushi (25) ambaye ni mfanyabiashara wa vipodozi kutoka Moshi, Bi. Magadalena Daniel Asei (37) mfanyakazi wa DHL mkazi wa Kigamboni-Dar es Salaam na Bi. Hilda Laurence Nyambo (56) ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Bima kutoka Kinondoni, Dar es Salaam.

Wengineni Bi. Maria JumaMbata (26) mhitimuwa Chuo Kikuu mkazi wa Iringa na Bw. Aloyce Idrisa Njole (23) mwanafunzi wachuo cha ufundi anayetoka mkoani Morogoro.

“Tigo inafuraha kubwa sana kwasababu imewezakuleta tabasamu katika nyuso za wateja wake katika kipindi hiki cha mwaka mpya. Tunaamini kwamba zawadi hizi zitawafurahisha na kuwa fanya washerehekee sikukuu hii ya kuuaga mwaka 2013 kuingia 2014 kwa namna yakipekee,” alisema Bi. Rutta.

Aliongeza, “Kwa ujumla zawadi zilizo shindaniwa jana ni milioni 50 kwa washindi watano waliopatikana, milioni 40 kwa washindi 20 na milioni 70 kwa washindi 350 ambapo kila siku wateja 50 walikuwa wanajishindia shilingi laki 2 kila mmoja, iliyofanya jumla kuwa shilingi milioni 160.”

Kwa mujibu wa Mratibu huyo wa Promosheni droo hii ilikuwa ya kuanzia tarehe 24 hadi 30 Desemba.

Utaratibu washindano hili unaruhusu wateja waliosajiliwa na Tigo Pesa kushiriki katika promosheni hii kwa kutuma fedha, kununua bidhaa kupitia Tigo Pesa, kutoa fedha, kununua muda wa maongezi au kulipia huduma mbali mbali kupitia Tigo Pesa. Promosheni hii itaisha Februari 12 mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment