Tuesday, 18 March 2014

Sio lazima photopoint, cheki mdau huyu aliyetoa pozi juu ya gari lilipokai godoro na makabati


Danger: Mdau adandia lifti nyuma ya lori la mafuta

Mkazi wa jiji la Dar es Salaam(jina halikufahamika) ambaye ni mmachinga akiwa amedandia nyuma ya lori la mafuta lenye alama ya tahadhari 'danger' eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam. 



Afya na mazingira, je ni sawa kuchoma taka barabarani?

Mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam akipita pembezoni mwa takataka zilizochomwa eneo linaloangaliana na kituo cha polisi cha kawe.
Vitendo hivi vya kuchoma takataka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam yakiwemo karibu na makazi ya watu pamoja na barabarani yamekuwa yakiendelea bila kujali afya za wapiti njia wala watu waliojirani na maeneo hayo. Swali lipo pale pale, je ni sawa kuchoma takataka barabarani na maeneo karibu na makazi ya watu?

Friday, 14 March 2014

Madereva Bodaboda waandamana makao makuu ya Chadema-Slaa azungumza nao

Moja wa dereva bodaboda akionesha bango lilioandikwa 'UKABAJI WIZI UTAONGEZEKA' wakati walipoandamana hadi makao makuu ya Chadema leo mchana ili kumsihi katibu mkuu wa chama hicho, Dr. Slaa awasilishe hoja yao yaruhusu bodaboda kuingia mjini baada ya agizo la mkuu wa mkoa kuwazuia madereva bodaboda hao wasiingie mjini. Dr. Slaa amewahidi kuzungmzia swala hilo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo watakutana siku ya jumatatu.(Picha zote: Atuza Nkurlu)
 
Katibu mkuu wa Chadema, Dr. Willibrod Slaa akizungumza na waendesha bodaboda leo mchana walipoandamana hadi makao makuu ya chama hicho ili kumsihi awasilishe hoja ayao ya kuruhusu bodaboda kuingia mjini baada ya agizo la mkuu wa mkoa kuwazuia madereva bodaboda hao wasiingie mjini. Dr. Slaa amewahidi kuzungmzia swala hilo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo watakutana siku ya jumatatu.
Katibu mkuu wa Chadema, Dr. Willibrod Slaa akizungumza na waendesha bodaboda leo mchana. Mamia ya madereva bodaboda walifika makao makuu ya Chadema, Kinondoni wakiwa na lengo la kupinga agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, lililowazuia maderva bodaboda kuingia mjini.

Mmoja wa dereva bodaboda akionesha tofauti kati ya risiti orijino na risiti feki wanazobambikiziwa na matrafiki jijini Dar es Salaam. 

Madereva bodaboda wakitawanyika baada ya kuongea na katibu mkuu wa Chadema, Dr. Willibrod Slaa.

Tamko la Vodacom kuhusu huduma ya internet kwenda taratibu


Vodacom Tanzania Managing Director, Rene Meza.
 
Eassy Subramine Cable  Damage….

Vodacom Customers Experience Slow Internet Speeds

Vodacom Tanzania’s internet users today experienced slow internet speeds which were caused by a cut on the Eassy Submarine Fibre cable  which carries the company’s data traffic through South Africa.

Speaking in Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Managing Director, Rene Meza said his company had no option but to route all its internet traffic through the Seacom Submarine Cable in the Indian Ocean in order to ensure that customers had continued access to the internet.

“As a result of this, customers will have experienced low internet and delays in the execution of other services which rely on the internet. We understand the inconvenience that this outage has caused them and would like to apologize to them and to ask for their patience and support while we work to restore our services,” said Meza.

 He went on to say that due to its location on the Southern tip of Africa, the Eassy submarine cable is designed to carry Vodacom’s internet traffic via the Atlantic Ocean whereas the Seacom one routes traffic via   the Indian Ocean adding that…” the two cables are also able to support each other in times of failure and that is why we are now carrying all our internet traffic through the former. This increased traffic load on the Seacom cable is slowing down our internet speeds as it is now carrying a far heavier load than it was originally designed to.”

With regards to what was being done to rectify the situation, Meza said, the Eassy technical team was working hard to assess the magnitude of the damage caused by the fibre cut at Mtunzini Bay which lies  29.5 kilometres off the shore of the Atlantic Ocean and to repair it.    

We would kindly like to request our esteemed customers to please bear with us as we continue to work to restore all our services. I would like to assure our esteemed customers that we at Vodacom remain committed to continue providing them with world-class services and our aim is to restore services as soon as possible,” says Meza

Thursday, 13 March 2014

Rais Kikwete kumwapisha Katibu wa Bunge maalumu la katiba kesho Dodoma


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 
Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya kesho, Ijumaa, Machi 14, atamwapisha Katibu wa Baraza la Wawakilishi Bwana Yahya Khamis Hamad kuwa Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.

Aidha, katika sherehe fupi itakayofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma, Rais Kikwete atamwapisha Katibu  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.

Taarifa iliyotolewa jioni ya leo, Alhamisi, Machi 13, mwaka huu wa 2014 mjini Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Rais Kikwete atawaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa kifungu cha 24(7) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014.

Bwana Hamad na Dkt. Kashilillah wanashika  nafasi hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 24(1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014, ambacho kinasema kuwa nafasi za Katibu na Naibu katibu wa Bunge Maalum la Katiba zitajazwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar.

Kwa mujibu wa kifungu cha 24(3) cha sheria hiyo, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014, Katibu wa Bunge Maalum atatoka upande tofauti na ule anakotoka Mwenyekiti wa Bunge Maalum.

Kwa vile aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mheshimiwa Samuel John Sita anatoka Tanzania Bara, basi Katibu wa Bunge anakuwa Bwana Yahya Khamis Hamad ambaye ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba anakuwa Dkt. Kashililah  ambaye ni Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwisho.

 

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

13 Machi,2013

 

Tuesday, 11 March 2014

WAZEE WA YOMBO KILAKALA WATOA YA MOYONI

Mhasibu wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Joyna Mwafute akimlisha  chakula mmoja wa wazee waishio katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo kilakala Bi.Tabu Juma( 65) wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipofika kituoni hapo kutoa misaada wa vyakula,mafuta ya kula,blanketi na mashuka vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5/-.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  wakiwa katika picha ya pamoja na wazee wasiojiweza wa kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation ilichopo Yombo Kilakala wakati walipokwenda kuwapa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka, blanketi,vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2.5/-.

.......................................................................................
WAZEE WALIA NA SERIKALI
 
Wazee wa Yombo Kilakala wameililia Serikali juu ya kukosa huduma stahiki kama ukosefu wa matibabu na matunzo bora kwasababu ya kunyanyapaliwa na kutelekezwa  na familia zao hivyo kuishi katika mazingira magumu.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na wazee waishio Yombo Kilakala wilayani Ilala jijini Dar es salaam  wanaofadhiliwa na Taasisi ya Tushikamane pamoja walipotembelewa  na Wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa Ajira ya Erolink  kwa lengo la kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu yenye zaidi ya shilingi milioni 2.5/-.
 
Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, Bi.Julietha Mchanga(90) alisema kuwa  changamoto kubwa nyowakabili ni  kukosa matunzo na matibabu yasiyostahili kwani wengi wao hawana msaada.
 

Bi. Mchanga alibainisha kuwa hayo yanatokana na kukimbiwa na  kutothaminiwa na watoto wao hivyo kukosa matunzo jamboa mabalo huwafanya wazee waishi maisha magumu.
 
Vilevile alisema kuwa sera ya kutunza wazee haitekelezwi ipasavyo hivyo ni wakati mwafaka kwa serikali na jamii kwa ujumla kutambua na kuwakumbuika kwani ni miongoni mwa watu waliosahaulika hapa nchini.
 
Mfanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Zabida Kibiki akimvisha shuka baada ya kumkabidhi msaada huo John Shitundu ambaye ni miongoni mwa wazee waliopo chini ya kituo chaTushikamane Pamoja Foundation wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa kituo hicho Rose Mwapachu.
Kwa upande wake, Taddious Ndyetabuula  ambaye ni Meneja mikataba wa kampuni ya Erolink Alisema kuwa  msaada walioutoa  kwa wazee hao  umekwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani lakini pia lengo kuu ni kujumuika na  wazee wasiojiweza  ili  wajione kwamba hawajasahaulika.
 
“Msaada huu wa vyakula,mafuta ya kupikia ,sabuni  na mashuka pamoja na hafla hii ya  kujumuika na wazee kwaajili ya chakula cha mchana ni endelevu ,hivyo sisi kama Erolink ni jukumu na wajibu wetu  kuhakikisha kwamba tunawasaidia na kuwathamini wazee wanaoishi katika mazingira magumu” alisisitiza Ndyetabuula.
 
Baadhi ya wazee wanaoishi na kutunzwa katika Kituo cha  Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,wakicheza pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  walipowatembelea wazee hao mahususi kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5/-.

Naye  Mwenyekiti  wa taasisi ya  Tushikamane Pamoja, Rose Mwapachu alisema kuwa  hana budi kuishukuru Kampuni ya Erolink kwa msaada walioutoa kwa wazee haoo lakini pia alitumia fursa hiyo kuyaomba mashirika na makampuni mbalimbali kuwaungamkono katika jitihada zao za kuhakikisha    ustawi wa maisha bora ya  wazee hapa nchini.
 
“Tuna utaratibu wa kutoa misaada ya kibinadamu  kwa wazee katika vituo mbalimbali jijini hapa ikiwemo kinondoni,manzese,tandale,magomeni na maeeo mengine lakini uwezo wetu ni mdogoi tunahitaji wafadhili zaidi kwaajili ya  kujenga majengo kuishi hawa wazee kwani wengine hawana makazi iantubidi kuwalipia kodi”Alisisitiza Mwapachu
 
Aliongeza kuwa hivi  sasa serikali imewapa kiwanja huko Kwembe (Nje kidogo ya jiji la Dar es salaam)na wapo katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi  lakini pi8a bado wanahitaji msaada zaidi iliwaweze  kukamilisha ujenzi huo ili waweze kuwatunza na kuwalea  wazee  katika mazingira mazuri.