UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya
kesho, Ijumaa, Machi 14, atamwapisha Katibu wa Baraza la Wawakilishi Bwana
Yahya Khamis Hamad kuwa Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.
Aidha,
katika sherehe fupi itakayofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma, Rais Kikwete
atamwapisha Katibu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu wa
Bunge Maalum la Katiba.
Taarifa
iliyotolewa jioni ya leo, Alhamisi, Machi 13, mwaka huu wa 2014 mjini Dodoma na
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Rais Kikwete
atawaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa
kifungu cha 24(7) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, toleo la
mwaka 2014.
Bwana
Hamad na Dkt. Kashilillah wanashika nafasi hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 24(1)
cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014, ambacho
kinasema kuwa nafasi za Katibu na Naibu katibu wa Bunge Maalum la Katiba
zitajazwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa
Baraza la Wawakilishi, Zanzibar.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 24(3) cha sheria hiyo, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014,
Katibu wa Bunge Maalum atatoka upande tofauti na ule anakotoka Mwenyekiti wa
Bunge Maalum.
Kwa
vile aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mheshimiwa Samuel John Sita
anatoka Tanzania Bara, basi Katibu wa Bunge anakuwa Bwana Yahya Khamis Hamad
ambaye ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar na Naibu Katibu wa Bunge
Maalum la Katiba anakuwa Dkt. Kashililah ambaye ni Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
13 Machi,2013
No comments:
Post a Comment