Mpiga tumba wa bendi ya Mashujaa akionyesha Ufundi katika kupiga ngoma wakati wa uzinduzi wa bendi ya Extra Bongo, “Mtenda akitendewa”. |
............................................................................................................................................
Dar es Salaam, Februari 24, 2014 … Ilikuwa ni siku ya aina
yake kwa bendi ya Extra Bongo "wazee wa kizigo" walipokuwa wakizindua
albamu yao ya mtenda akitendewa na kuacha gumzo kwa mamia ya mashabiki
waliojitokeza ukumbini humo asante kwa udhamini wa Vodacom kufanikisha Tamasha
hilo.
Palikuwa hapatoshi katika ukumbi huo wa taifa wa burudani wa Dar
Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo bendi kaadhaa za muziki wa
dansi na wasanii wa bongo flava zilitumbuiza kabla ya uzinduzi wenyewe
kufanyika.
Kivutio kikubwa zaidi kilikuwa ni pale ambapo kiongozi wa bendi
ya Extra Bongo, Kamarade Ali Choki alipoingia na gari ya kubebea wagonjwa
(Ambulance) ukumbini kutumbuiza mashabiki wake waliofurika kwa wingi.
Uzinduzi wa albamu hiyo iliyokwenda kwa jina la Mtenda
akitendewa ulikwenda sambamba na burudani lukuki kutoka kwa wanamuziki mbali
mbali mashuhuri nchini kama vile malikia wa mipasho nchini Khadija Omari Kopa,
Banza Stone, Abdul Misambano, Mashujaa Band pamoja na wasanii wa bongo flava
Linah na Amini ulidhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom.
Wanenguaji wa Extra Bongo walifanikiwa vilivyo kuzikonga nyoyo
za mashabiki ukumbini hapo kwa kupagawisho vilivyo jukwaani kwa staili mbali
mbali mpya za uchezaji.
Kwa upande wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wa bongo
flava, Linah na Amini walidhibitisha kwa nini wao ni waimbaji bora na
wataendelea kuwa hivyo kwa kuonyesha kipaji cha hali ya juu katika kulimiliki
jukwaa ambapo waliimba kibao chao kitamu cha ‘Omotima wange ni wewe’.
No comments:
Post a Comment