Kocha Mkuu wa Manchester United, David Moyes(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jioni jijini Athens ambapo timu hiyo inatarajia kucheza mechi na Olympiacos katika ligi ya Mabingwa kesho. |
Jonny Evans |
Wachezaji wa Manchester United, Phil Jones na Jonny Evans hawajasafiri kuelekea Ugiriki kucheza ligi ya Mabingwa(UEFA Champions league) raundi ya 16 dhidi ya timu ya Olympiacos.
Mabeki hao wawili wamekosa mechi kadhaa baada ya kuumia kwenye mechi
waliyocheza na Stoke City, February 1 ambapo United walitoka sare ya 2-2. Jones alipata jeraha la kichwa baada ya kugongana na Jonathana Walters wakati Evans aliumia misuli ya nyuma ya
goti.
Phil Jones |
Katika mkutano na waandishi wa habari leo jioni jijini Athens, David
Moyes alithibitisa kukosekana kwa wachezaji hao wawili na kueleza jinsi anavyotarajia
kukumbana na timu ya kigiriki, Olympiacos katika kiwanja cha Karaiskakis.
“Jones na Evans hawajasafiri nasi, wachezaji wengine wote tupo nao,” alisema
Moyes kwa waandishi wa habari. “Nilipata bahati ya kuangalia mechi ya Arsenal
na Bayern Munich na kufurahia ligi ya Mabingwa."
Akizungumza kuhusiana na ligi hiyo Moyes alisema, “Kupata nafasi
ya kuingia ilikuwa ni kitu muhimu cha kwanza. Kushinda kwenye kundi ni
nyongeza. Natarajia hilo. Ni kweli ni mchezo mgumu, Olympiacos wanarekodi nzuri
hapa, na tunafahamu, katika rekodi yetu tunasare hivyo tunabidi tucheze vizuri ili tuweze kufuzu.” Aliongezea
Moyes.
Kocha huyo wa
Manchester United pia alisema Olympiacos walifanya vizuri dhidi ya PSG na
Benfica ambapo walitoka kwenye kundi gumu sana. Alisema wanafahamu kuwa utakuwa ni usiku mgumu sana dhidi ya Olympiacos kwasababu wanamsaada mkubwa kwani wapo nyumbani hivyo
mechi hiyo haitakuwa rahisi.
No comments:
Post a Comment