TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko taarifa za tukio la kutekwa, kuteswa na
kuumizwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick.
Chama kupitia
Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano, mbali ya kukemea kwa nguvu zote tukio
hilo la kihuni na mengine ya namna hiyo yenye lengo ya ukatili dhidi ya
binadamu, katika hatua ya sasa kinapenda kusema yafuatayo juu ya tukio hilo ovu
;
1.
Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi
juu ya tukio hilo la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya
Temeke ili ukweli ujulikane na haki itendeke, kwa sheria kuchukua mkondo wake.
2.
Chama kinawataka wanachama na Watanzania kwa
ujumla kutulia, hasa pale ambapo watu wenye hila na malengo yao, wanaanza
kukihusisha chama na tukio hilo. Watambue kuwa pamoja na mtu yeyote kuwa
kiongozi wa chama, bado anayo maisha yake na uhusiano na watu wengine katika
jamii.
3.
Jeshi la Polisi linapaswa kuyachukulia uzito
mkubwa na unaostahili matukio ya namna hii ambayo yanaanza kuota mizizi
kutokana na watu waovu wanayoyatekeleza kutochukuliwa hatua za kisheria ambazo
zingesaidia kuzuia yasitokee tena.
4.
Watanzania bado wanakumbuka kwamba
hadi sasa Jeshi la Polisi limeshindwa kutoa taarifa za kina na kuchukua hatua
za kisheria ambazo zingesaidia ukweli kujulikana na haki kutendeka katika
matukio ya kutekwa na kuteswa kwa kiongozi wa madaktari Dk. Steven Ulimboka na
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda. Hivyo ingesaidia kuzuia
matukio mengine kutokea.
5.
Ni kutokana na jeshi hilo kushindwa
kuwajibika ipasavyo katika matukio mengine ya namna hiyo, watu waovu wanaweza
kutumia mwanya wa kinachoendelea ndani ya CHADEMA kwa chama kuchukua hatua za
kinidhamu dhidi ya wanachama wasio waadilifu, kufanya matukio ya namna hiyo ili
kujenga taswira ya kukihusisha chama na uhuni huo unaobeba kila sifa ya kuitwa
ukatili dhidi ya binadamu.
6.
Aidha kushindwa kwa Jeshi la Polisi kuwajibika
ipasavyo katika kufanya uchunguzi wa matukio hayo (yaliyotolewa kama mfano hapo
juu) na mengine ya namna hiyo, jeshi hilo linazidi kujiweka katika wakati mgumu
wa kukwepa tuhuma za baadhi ya watendaji wake kujua na kushiriki masuala haya,
hususan kwa kurejea tukio la kutekwa kwa Dkt. Ulimboka.
Asubuhi ya leo MillardAyo.com iliripoti kwamba Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam.
Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’.
No comments:
Post a Comment