Monday, 6 January 2014

WILL Smith avunja ukimya juu ya kifo cha actor James Avery maarufu kama 'Uncle Phil'

James Avery maarufu kama 'Uncle Phil' alifariki ghafla wiki iliyopita kutokana na matatizo aliyopata baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. Watu wengi walishatuma salamu zao za rambirambi kuhusiana na kifo cha staa huyo kupitia mitandao malimbali, ila cha kushangaza ni kwamba Will Smith aliyeonekana kuwa na mahusiano ya karibu sana na Phil hapo awali, hakusema chochote.

Hatimaye, Will Smith amevunja ukimya juu ya kumpoteza 'Uncle' wake wa kwenye uigizaji na kuweka picha na kusema maneno machache chini yake. Will alifunguka kupitia ukurasa wake wa facebok akieleza kuguswa kwake na kifo hicho. Aliweka picha ya kundi Zima lilioact Fresh Prince of Bel Air wakiwa ni watu wazima sasa ambapo kutokana na maelezo ya picha, hiyo ndiyo picha ya mwisho waliopiga pamoja.

Some of my greatest lessons in acting, living and being a respectable human being came through James Avery. Every young man needs an Uncle Phil. Rest in Peace.
'This photo was the last time we were together.'
Hayo ndiyo maneno ya Will Smith kwa marehemu Uncle Phil.

No comments:

Post a Comment