Tuesday, 7 January 2014

MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI, ZITTO KABWE ASHINDA KESI YAKE LEO MAHAKAMA KUU.

-UONGOZI WA CHADEMA WAPIGWA 'STOP' KUHUSU KUJADILI UANCHAMA WAKE.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akisindikizwa na bodyguard leo alipokuwa akitoka mahakamani baada ya kesi yake kuamuliwa. 

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam leo imetoa uamuzi kuhusu swala la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe ikisema uongozi wa Chadema hauruhusiwi kujadili swala lolote kuhusu uanachama wa Zitto Kabwe.
Jaji wa Mahakama Kuu aliieleza mahakama kuwa mlalamikaji anayo haki yakusikilizwa kama mwanachama yeyote, hivyo kuagiza wadhamini na uongozi wa wanachama hicho kuheshimu amri ya mahakama mpaka pale kesi ya msingi itakapoisikilizwa.
Kesi hiyo iliendeshwa zaidi ya saa 3 huku ikivuta hisia za mamia ya wakazi wa Dar es Salaam waliyokaa nje ya mahakama hiyo kusubiria hatma ya kada huyo. Kesi inatarajiwa kusikilizwa tena tarehe 13 mwezi huu wa January 2013.
                                   *Alichotweet Zitto Kabwe baada ya kushinda kesi hiyo*
 

No comments:

Post a Comment