Sunday, 12 January 2014

BENKI ya Covenant yazindua huduma ya 'Benki Mtaani Kwako'

Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya Covenant Balozi.Salome Sijaona(katikati)akibonyeza kitufe cha kopyuta kuashiaria uzinduzi rasmi wa huduma ya” benki mtaani kwako”. Anaeshuhudia kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bi.Sabetha Mwambenja pamoja na wajumbe  wa bodi wa benki hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya Covenant Balozi.Salome Sijaona(kulia)akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bi.Sabetha Mwambenja.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant Bi.Sabetha Mwambenja(katikati)akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya” Benki Mtaani Kwako”. Pamoja nae katika picha ni  Mwenyekiti wa Bodi wa benki  hiyo Balozi.Salome Sijaona(watatu kutoka kushoto) pamoja na wajumbe  wa bodi wa benki hiyo.
.......................................................................................................................................................

         Dar es Salaam. Katika kuhakikisha inaendelea kupanua wigo na kusogeza huduma zake za kibenki karibu na wateja  wake benki ya Covernant imezindua huduma za kibenki kwa njia ya simu inayojulikana kama”Benki Mtaani kwako” huduma hii ambayo itawawezesha wateja wa benki hiyo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao kupitia simu za Mkononi.
         Akizungumza  wakati wa kuzindua huduma hiyo Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Balozi.Salome Sijaona,amesema kuwa benki yake inawalenga watu wa kawaida kabisa ambao wengi wao wanaishi maeneo ya nje ya mji wengi wao wakiwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo hivyo kuanzisha huduma hii ni faraja kubwa kwa wateja wetu ambao hawatapata tabu tena ya kutoka sehemu waliko kuja katika tawi la benki hiyo kupata huduma.
        “Uzinduzi huu umekuja wakati muafaka ikiwa ni sehemu muhimu ya kuendelea kuboresha na kusogeza huduma zetu kwa wateja wetu, tuna wateja maeneo mengi ya mjini na vijijini, tumeona ni jambo jema kuwaanzishia huduma hii ambayo haita walazimu wao kuja katika tawi letu kupata huduma, aliongeza  Balozi Sijaona.
         “Tunawajali na kuwathamini wateja wetu na sasa tumewaletea huduma hii ya  kuweka na kutoa pesa kwenye akaunti zao kupitia simu za kiganjani wakiwa mahala popote pale, wote tunatambua kuwa dunia ya sasa teknolojia ndio kila kitu, mtu anapoweza kupata kila kitu kupitia simu yake ya mkononi ni jambo jema kwetu, natoa wito kwa wateja wetu kutumia huduma hii ambayo naamini ni suluhisho kwao watakapo kuwa na uhitaji wa kuweka au kutoa fedha katika benki yetu.”
          Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bi. Sabetha Mwambenja amesema amefurahi kwa benki yake kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wake na kuhakikisha wanafikia malengo ya huduma bora kwa wateja wake,Pia alizitaja sifa muhimu za huduma hiyo kuwa ni kulipia Ankara mbalimbali,kuhamisha fedha kwenda akaunti yoyote uliyokuwa nayo na covenant benki,kuhamisha fedha kupitia mtandao wowote wa simu za viganjani nchini,kutuma na kuchukua fedha ATM bila kadi ya benki hata kama aliyekutumia hana akaunti na Covenant benki,kupata miamala uliyofanyika kwenye akaunti yako na kusajili huduma hii mwenyewe kupitia simu yako na usajili unakamilika papo hapo.
           “Tunamipango mingi ya kuendelea kupanua na kuboresha huduma zetu, hadi kufikia sasa tunashukuru namna ambavyo wateja wetu wameendelea kutuunga mkono siku hadi siku, tunawaahidi kuendelea kuwaunga mkono na kuhakikisha tunatimiza ndoto zao za kuwa na maisha bora.”
           Tunaendelea kuwahamasisha Watanzania kuendelea kujiunga na huduma zetu ambazo zinafaida nyingi kwani wateja wanaweza kutumia akaunti zao wakati wowote,kuondoa adha ya kusafiri/kutembealea tawi la benki,kuhamisha fedha kwa uwapendao kwa urahisi zaidi,wanaweza kuwalipa washiriki wa biashara na wagavi bila wasiwasi,Pia hadi sasa tunazo akaunti za aina mbalimbali ambazo ni akaunti za akiba inayojumuisha akaunti ya Ahadi, Jerusalem, Tausi Women Entrepreneurs Account, Winner Junior account, Vikundi, Akaunti ya Akiba ya Bajaj, Akaunti ya Muda Maalum na nyinginezo na akaunti za biashara ni pamoja na akaunti binafsi na nyinginezo.
         Ili kujiunga na huduma hiyo Mteja wa benki hiyo atatakiwa kupiga namba *150*27#
 

No comments:

Post a Comment