Wateja wa Tigo wakijaza fomu kwa ajili ya kusajili namba zao za simu mara baada ya duka hilo jipya kufunguliwa. Duka hili la Tigo linapatikana Mbagala, Zakhiem kwenye sheli ya Big Bon. |
Wateja wa Tigo wakiendelea kupatiwa huduma mbali mbali. Tawi hilo linakariwa kuhudumia watu zaidi ya 300 kwa siku. |
...............................................................................................................................................................
Dar es Salaam. Tigo imefungua duka jipya la huduma kwa wateja lililopo Mbagala jijini Dar es Salaam ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake kwa wateja wa eneo hilo na vitongoji jirani ambao awali walikuwa wakienda katikati ya jiji kupata huduma za kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, Meneja Uendeshaji wa Huduma kwa Wateja wa Tigo, Eliud Rugemalira, amesema tawi hilo jipya ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo wa kufikisha huduma zake karibu zaidi na wateja.
Rugemalira amesema tawi hilo lintarajia kuwahudumia wateja wapatao 300 kwa siku kwa kuwapa huduma mbali mbali za Tigo zikiwemo huduma ya kuunganishiwa intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma maalum za simu za kisasa (“Smartphones”).
“Duka hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu limeleta huduma zetu karibu zaidi kwao. Pia linapatikana sehemu nzuri kibiashara kiasi kwamba litavutia hata wateja kutoka maeneo jirani kama Temeke, Kongowe, Zakiemu na Mkuranga kuja kuhudumiwa hapa,”alisema.
Duka hili linatoa huduma nyingine maalum zikiwemo uuzaji wa bidhaa mbali mbali kama simu za kisasa ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribisha kabla ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi katika kuchagua na kununua bidhaa inayokidhi mahitaji yake.”
Tawi la Mbagala linafikisha jumla ya maduka yanayoendeshwa na kampuni ya Tigo jijini Dar es Salaam kuwa 13. Kwa mujibu wa Rugemalira, kampuni hiyo ina mipango ya kufungua maduka mengine mengi zaidi katika sehemu mbali mbali nchini.
No comments:
Post a Comment