Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni washindi wa droo ya tatu ya Tigo 'Shinda kitita na Tigo Pesa' Nassoro Yusuphu(kushoto) na Nuru Staford. |
Dar es
Salaam, Januari 13, 2014 – Tigo
imekabidhi jumla ya zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi milioni 400
ndani ya mwezi mmoja katika promosheni yake ya ‘Cheza Kwa Furaha Unaposhinda
Kitita na Tigo Pesa’ huku fedha zingine 720 milioni zikibakia kushindaniwa.
Akizungumzia muenendo wa promosheni hiyo leo jijini Dar es
Salaam, Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa Mary Rutta alisema kwamba jumla ya
zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya bilioni 1.12 zitashindaniwa na
watumiaji wa Tigo Pesa mpaka pale promosheni hiii itapofikia ukomo katikati ya
mwezi wa Februari.
Rutta alisema tayari wateja 1,215 kutoka kila mkoa nchini
ameweza kujishindia zawadi hizi akiongeza, “tunatarajia idadi kubwa zaidi ya
wateja wa Tigo Pesa kushinda katika mwezi unaokuja ya kampeni yetu ambayo bado
jumla ya shilingi milioni 720 zimebakia kushindaniwa.”
“Tunaendelea kutoa wito kwa wateja wetu wa Tigo kuendelea
kufanya miamala ya Tigo Pesa kadri wawezavyo katika muda huu uliobaki wa
promosheni ili waweze kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda,” alisema Rutta.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mratibu wa
Promosheni wa Tigo Pesa pia alikabidhi zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya
shilingi milioni 110 kwa washindi wengine 375 walioshinda kwenye droo ya
promosheni hiyo wiki iliyopita, ambapo washindi 20 walijishindia shilingi
milioni 2 kila mmoja na wengine 350 pia walijinyakulia shilingi laki 2 kila
mmoja.
Washindi watatu waliokuwepo katika makabidhiano hayo
walisema kwamba wamefurahi sana kushinda fedha hizo taslimu na kuahidi kwamba
watatumia fedha hizo kuboresha maisha yao.
Anachohitaji kufanya mteja ili kuingia kwenye droo, alisema
Rutta, ni kutumia akaunti yake ya Tigo Pesa kutuma fedha, kununua bidhaa,
kuongeza salio au kulipia bili mbali mbali.
No comments:
Post a Comment