Mtaalam wa Huduma kwa wateja kutoka Tigo, Henry Mboya(kulia) akionesha
jinsi mashine maalumu ya ‘TigoMatic’ inavyoweza kutumika mara baada ya uzinduzi wa
mashine hizo leo jijini Dar es Salaam.
Pembeni ni Mkuu wa Idara ya Huduma kwa wateja, Zaem Khan.
Dar es Salaam, Desemba 24, 2013. Tigo Tanzania leo
imetangaza uzinduzi wa mashine maalum zinazowawezesha wateja wake kupata huduma
za kutuma na kupokea fedha, kulipia bili za huduma mbali mbali, kuongeza salio
na kupata laini mpya za simu zinazofanya kazi masaa ishirini na nne kwa siku.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika tafrija ya uzinduzi wake leo
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez alisema
kwamba mashine hizo zinazoitwa ‘TigoMatic’ zitawahudumia wateja aina wote,
ikiwemo wateja wa malipo ya kabla na wateja wa malipo ya baadaye, zikifanya kazi
masaa ishirini na nne kwa huduma zitolewazo na kampuni hiyo ya simu.
“Hakutakuwa na ulazima tena kwa wateja wetu kukaa kwenye foleni kwa
ajili ya kupata huduma zetu kutoka kwenye matawi yetu na sehemu zetu mbali
mbali za mauzo kwa sababu mashine hizi zitatoa msaada wa mteja kujihudumia
mwenyewe,” alisema Bw. Gutierrez.
Alisema kwamba wateja wa Tigo hawatakuwa na ulazima wa kujisajili upya
kwa ajili ya kutumia mashine hizo.
Akielezea jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi, Bw. Gutierrez alisema
kwamba Tigomatic ni mashine ambazo mteja anaweza akajihudumia yeye mwenyewe kama vile huduma za ATM ambapo mtu anaweza akafanya
miamala tofauti tofauti bila kuhitaji kumtegemea mfanyakazi wa benki.
Tigo ikiwa na wateja zaidi ya milioni 6 nchi nzima, Bw. Gutierrez
amesema kwamba mashine hizo zitatolewa kwa awamu kuanzia Dar es Salaam siku ya
leo (24 Desemba) kuelekea mikoa mengine mwakani. Mashine hizo zitawekwa katika
sehemu za mikusanyiko mikubwa ya watu kwa mfano kwenye maduka makubwa, stendi
za mabasi, barabarani, viwanja vya michezo na mahospitalini.
|
No comments:
Post a Comment