Friday 14 March 2014

Madereva Bodaboda waandamana makao makuu ya Chadema-Slaa azungumza nao

Moja wa dereva bodaboda akionesha bango lilioandikwa 'UKABAJI WIZI UTAONGEZEKA' wakati walipoandamana hadi makao makuu ya Chadema leo mchana ili kumsihi katibu mkuu wa chama hicho, Dr. Slaa awasilishe hoja yao yaruhusu bodaboda kuingia mjini baada ya agizo la mkuu wa mkoa kuwazuia madereva bodaboda hao wasiingie mjini. Dr. Slaa amewahidi kuzungmzia swala hilo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo watakutana siku ya jumatatu.(Picha zote: Atuza Nkurlu)
 
Katibu mkuu wa Chadema, Dr. Willibrod Slaa akizungumza na waendesha bodaboda leo mchana walipoandamana hadi makao makuu ya chama hicho ili kumsihi awasilishe hoja ayao ya kuruhusu bodaboda kuingia mjini baada ya agizo la mkuu wa mkoa kuwazuia madereva bodaboda hao wasiingie mjini. Dr. Slaa amewahidi kuzungmzia swala hilo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo watakutana siku ya jumatatu.
Katibu mkuu wa Chadema, Dr. Willibrod Slaa akizungumza na waendesha bodaboda leo mchana. Mamia ya madereva bodaboda walifika makao makuu ya Chadema, Kinondoni wakiwa na lengo la kupinga agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, lililowazuia maderva bodaboda kuingia mjini.

Mmoja wa dereva bodaboda akionesha tofauti kati ya risiti orijino na risiti feki wanazobambikiziwa na matrafiki jijini Dar es Salaam. 

Madereva bodaboda wakitawanyika baada ya kuongea na katibu mkuu wa Chadema, Dr. Willibrod Slaa.

No comments:

Post a Comment