Saturday, 18 January 2014

ALA KIPIGO KWA KUIBA MBWA NA DELI KAWE

Wakazi wa kawe wakimpa kipigo mwizi waliyemkamata akiiba mbwa na deli(kifaa cha kuhifadhia vimiminika ili visipoe)  jana usiku mitaa ya Kawe sokoni jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa kawe wakimpeleka kituo cha polisi cha kawe mtuhumiwa aliyekamatwa akiiba mbwa na deli(kifaa cha kuhifadhia vimiminika ili visipoe) mitaa ya kawe sokoni jana usiku jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa kawe wakimpeleka kituo cha polisi cha kawe mtuhumiwa aliyekamatwa akiiba mbwa na deli(kifaa cha kuhifadhia vimiminika ili visipoe) mitaa ya kawe sokoni jana usiku jijnii Dar es Salaam.
.........................................................................................................
Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, alijikuta akila kipigo  kutoka kwa wakazi wa kawe hadi kulia machozi baada ya kukamatwa akiwa ameiba mbwa na deli(kifaa cha kuhifadhia vimiminika ili visipoe) jana kawe sokoni jijini Dar es Salaam.

Kijana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 18-25 alikamatwa mida ya saa tano usiku ambapo wakazi wa kawe wenye hasira kali walimpa kipigo kabla ya kumfikisha kituo cha polisi cha kawe kilichopo jirani na mwizi huyo alipokamatiwa.

Vitendo vya wizi jijini Dar es Salaam vimeshamiri hususani kwa vijana wengi kujiingiza kwenye tabia hii ya wizi kutokana na kile kinachosemekana ni ugumu wa hali ya maisha. 

WAZIRI MKUU AKAGUA MAREKEBISHO YA UKUMBI WA BUNGE KWA AJILI YA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo ikiwa ni maandalizi ya Bunge la katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao.(Picha: PMO)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa ameketi kitini wakati akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo ikiwa ni maandalizi ya Bunge la katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao.(Picha: PMO)

Tuesday, 14 January 2014

NYAMA CHOMA FESTIVAL BACK AGAIN IN 2014


KWA mara ya kwanza kabisa mwaka huu 2014, lile tamasha kubwa la Nyama Choma linalofahamika kama The Nyama Choma Festival (TNCF) limepangwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 8 mwezi Machi, 2014.

Nani alifikiria kuwa Nyama choma ingeweza kuwaleta maelfu ya watu pamoja? Toka lilipoanzishwa, tamsha la Nyama Choma ambalo limesajiliwa kisheria limekuwa ni sehemu ya kipekee ya kuweza kufurahia aina mbalimbali za nyama choma na pia limekuwa ni eneo la kuwakutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali wanaofika kufaidi nyama zinazochomwa na wataalamu wa kuchoma nyma kutoka katika kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kwa kiingilio cha shilingi elfu 10,000 tu.
























 
Ukiachana na aina mbalimbali ya nyama zinazokwepo katika tamsha hili, pia ni sehemu mojawapo ya kufurahia na marafiki ikiwa ni pamoja na “mtoko” kwa familia kwani huduma zinazotolewa zimezingatia umri wa watu wote yaani kuanzia watoto hadi watu wazima. Kuna eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya michezo a watoto, vinywaji vya aina zote na burudani nzuri ya muziki. Si hivyo tu wapo watu wengine wanaotoa huduma ya kahawa, ice cream, michoro ya usoni, vyakula vya kawaida na michezo ya nje ya watu wazima kama vile pool n.k


Mwaka huu THE Nyama Choma Festival imeamua kuongeza wigo wake zaidi katika sehemu mbalimbali nchini. Ukiachana na Dar es Salaam TNCF ilishafanyika Moshi, Ausha na Mwanza na mwaka 2014 itaendelea katika mikoa ifuatayo ambapo tarehe zinaweza kubadilika.


-Dar es Salaam 08 March 2014

-Arusha 26 April 2014

-Mwanza 4 May 2014

-Dar es Salaam 6 September 2014

-Mwanza 26 October 2014

-Dar es Salaam 6 December 2014

-Moshi 26 December 2014
                                                                                                                                                                                              Kwa Habari Zaidi Othman Michuzi

UNDP:Tanzania yaongoza katika Mpango wa Majribio wa Mageuzi wa UN

Mwakilishi mkazi na Mratibu wa Shughuli za Umoja wa Mataifa nchini(Resident Coordinator of the UN System) Bwana Alberic Kacou akimfafanulia jambo Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu nakala ya Ripoti ya mwaka Utendaji ya (UNDP) 2012-2013 wakati mwakilishi huyo alipokwenda kumuaga Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo. Bwana Kacou anaondoka baada ya muda wake wa utumishi kumalizika hapa nchini(Picha: Freddy Maro)

Mwakilishi mkazi na Mratibu wa Shughuli za Umoja wa Mataifa nchini(Resident Coordinator of the UN System) Bwana Alberic Kacou akiagana na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo baada ya muda wake wa utumishi kumalizika hapa nchini. Dk. Kacou ameitumikia UN katika Tanzania kwa miaka minne unusu. (Picha: Freddy Maro)
..............................................................................................................................................................

Tanzania imefanya vizuri zaidi na kuonyesha mafanikio zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani kati ya nchi nane ambazo zilikuwa zinashiriki katika Mpango wa Majaribio wa Kuuwezesha Mfumo wa Umoja wa Mataifa Kufanya Kazi kwa Pamoja wa Delivering as One ambao sasa umepanuliwa kushirikisha nchi nyingi zaidi baada ya kuonyesha faida kubwa.
        Hayo yamesemwa leo, Jumanne, Januari 14, 2014,  na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN Resident Coordinator) katika Tanzania, Dk. Alberic Kacou wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,  Ikulu, Dar es Salaam.
       
       Dk. Kacou ambaye alikuwa anaagana na Rais Kikwete baada ya kuitumikia UN katika Tanzania kwa miaka minne unusu ameondoka nchini baadaye leo adhuhuri kwenda Makao Makuu ya UN, New York, Marekani, ambako atakuwa Mkuu wa Utawala (Chief of Staff) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Utawala na uendeshaji wa UNDP.
        
        Katika mazungimzo yao na Rais Kikwete, Dk. Kacou amemwelezea Rais Kikwete mafanikio ambayo yaliyopatikana katika mahusiano ya UN/UNDP na Tanzania katika miaka minne iliyopita ikiwa ni pamoja na shirika hilo la Umoja wa Mataifa kuunga mkono kifedha na kiufundi shughuli za uchaguzi mkuu katika Tanzania.
       
        Kuhusu mpango wa Delivering as One ambao unalenga kuuwezesha Umoja wa Mataifa kuwa na ufanisi zaidi na kutoa huduma kwa haraka na ubora zaidi na kupunguza matumizi, Dk. Kacou amemwambia Rais Kikwete:
     
      “Tanzania imetoa mchango mkubwa sana katika mageuzi yanayofanyika ndani ya UN ya Delivering as One kiasi cha kwamba nchi yako, Mheshimiwa Rais, imeongoza miongoni mwa nchi nane ambako majaribio ya mfumo huo mpya yalikuwa yanafanyika. Serikali yake imeonyesha kiwango cha juu sana cha kuyakubali na kuyaongoza majaribio hayo. Matokeo yake ni kwamba mpango huo sasa unapanuliwa na kuanza kufanya kazi katika nchi nyingine 45 duniani.”
 
          Dk. Kacou amesifia sana amani na utulivu wa Tanzania na kusema kuwa sifa hizo ndizo zinaendelea kuifanya Tanzania nchi ya mfano katika eneo ambako amani na utulivu ni tunu za nadra sana.

            Naye Rais Kikwete amemwambia Dk. Kacou: “Tunakushukuru sana. Wakati wa uongozi wako, uhusiano wa Tanzania na UN umeimarika sana na nchi yetu imenufaika sana na hali hiyo ya kuimarika kwa uhusiano. Uongozi wako umekuwa wa mfano kabisa na ni matarajio yetu kuwa mrithi wako ataendeleza mazuri mengi ambayo unayaacha nyuma.”
 
Ameongeza Rais Kikwete: “Umekuwa mmoja wa viongozi bora zaidi wa UNDP katika nchi yetu. Chini yako, UNDP imesaidia kuleta uwiano bora zaidi baina ya taasisi mbali mbali za kimataifa na za Umoja wa mataifa. Chini yako, UNDP imekuwa ni sauti ya busara katika dunia ambako busara ina mipaka yake.”
         “Tunathamini sana mchango wako katika maendeleo ya Tanzania. Tunathamini juhudi zako na mafanikio yako katika miaka yako minne ya uongozi bora wa UNDP katika nchi yetu. Tunakutakia heri na mafanikio makubwa katika kazi yako mpya na katika maisha yako ya baadaye. Umethibtibisha kuwa wewe ni binadamu bora na ofisa bora wa Umoja wa Mataifa.”

Imetolewa na;
Kurugenzi ya mawasiliano, Ikulu.

Monday, 13 January 2014

NYOTA wa Madrid, Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia-2013( FIFA Ballon d'Or)

Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiwa amebeba tuzo yake ya uchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2013 kwenye halfa hiyo ya Fifa Ballon d'Or iliyofanyika jumatatu Zurich-Uswisi. Ni mara ya pili kwa mchezaji huyo wa Ureno kujinyakulia tuzo hiyo baada ya kushinda mwaka 2008 akiwa akiichezea timu ya Manchester United.
 

Cristiano Ronaldo akijipangusa machozi baada ya kupanda stejini kwa ajili ya kupokea tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2013. Akimpongeza ni nyota wa Zamani, Pele.
 

Cristiano Ronaldo na mwanae amabye pia anaitwa Cristiano aliyeongozana nae kupokea tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2013 katika halfa ya Fifa Ballon d'Or iliyofanyika Zurich-Uswisi.
Cristiano Ronaldo na mpenzi wake, Irina Shayk wakiwa kwenye tuzo ya ifa Ballon d'Or Zurich-Uswisi.
Lionel Messi na mkewe, Antonella.
Nyota wa zamani wa Brazil, Ronaldo Delima akiwa na mkewe kwenye tuzo za Fifa Ballon d'Or Zurich-Uswisi.

Zidane akimpongeza Franck Ribbery.

ZURICH , Uswisi - Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2013(FIFA Ballon d'Or), na kusimamisha mbio za Lionel Messi alieshinda tuzo hizo kama mchezaji bora wa dunia kwa miaka minne mfurulizo.

Ronaldo alifunga mabao 69 kwa Real Madrid na Ureno mwaka jana, na kufunga Hat-trick ya ajabu dhidi ya Sweden katika mchujo wa Kombe la Dunia zitakazo chezwa Brazil.

"Hakuna maneno yatakayoweza kueleza wasaa huu," alisema Ronaldo, ambaye alionekana akitokwa na machozi baada ya kupokea tuzo hiyo akiwa na mtoto wake mdogo, ambaye pia jina lake ni Cristiano.

Ronaldo amewashinda Messi(Barcelona) na winga wa Ufaransa(Franck Ribery), anayeichezea timu ya Bayern Munich.

Upigaji wa kura ili kupata mshindi ulifanyika na makapteni wa timu ya taifa, makocha, pamoja na baadhi ya waandishi wa habari walioteuliwa, katika nchi FIFA ya 209 wanachama ambao waliamua juu yao -3 upendeleo.

Kura hizo zilionesha Ronaldo kupokea pointi 1365 , huku Messi alikuwa na pointi 1205 na Ribery akipata pointi 1127.
Kocha wa Canada, Benito Floro alitupa kura yake ya kwanza kwa Ronaldo, wakati nahodha Atiba Hutchinson atupa kura yake ya kwanza kwa Messi na Ronaldo ya pili .

Ronaldo alionekana akifunga macho yake wakati nyota wazamani wakibrazil, Pele aliposoma jina lake huku akitabasamu.
Roanldo alimbusu mpenzi wake, Irina Shayk , kabla ya kupanda stejini kwa ajili yakupokea tuzo hiyo.

"Watu ambao wananijua wanafahamu watu wangapi wamenisaidia , " alisema mshindi huyo kwa hisia katika lugha ya kireno.
Akiongeza "Kama nimemsahau mtu yeyote naomba anisamehe."

Ronaldo alisubiri kwa mda wa miaka mitano tangu kushinda tuzo ya kwanza kama mchezaji bora wa dunia mwaka 2008 akiwa anachezea timu ya Manchester United, kwa kuwa Messi alikuwa akimpiku kwa miaka minne mfurulizo.

HAKUNA ukweli hata mmoja katika tuhuma dhidi ya Freeman Mbowe-CHADEMA

                                            TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE

Freeman Mbowe








Nimrod Mkono






Kama mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wanaotaka kuhamisha mjadala wa makosa yanayowaandama ya utovu wa maadili na usaliti dhidi ya chama, hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amezushiwa tuhuma zisizokuwa na ukweli wowote zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya uongozi na kuipaka matope taasisi anayoiongoza;

Tuhuma hizo ni pamoja na;

1.     Kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40 ili Mwenyekiti Mbowe asifanye kampeni katika jimbo hilo.
2
.     Mwaka 2008, eti Mbunge Mkono alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni 20 kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Tarime, kisha akazitoa kwenye chama kama mkopo na akalipwa.

3.     Mwaka 2010, wakati wa uchaguzi mkuu Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili ya kampeni za mgombea urais.

4.     Mwaka huo huo wakati wa uchaguzi mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa, alipokea sh. Milioni 100 kutoka kwa Rostam Aziz kwa ajili ya kampeni.

Idara ya Habari ya CHADEMA, inapenda kusema yafuatayo;

1.     Hakuna ukweli hata mmoja katika tuhuma hizo. Ni uongo na uzushi uliopangiliwa kama moja ya mikakati ya watu wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii kwamba viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na wale wa CCM na kwamba chama hiki kikuu cha upinzani kinachobeba matumaini ya Watanzania katika kupigania haki zao na kupinga kila aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi.

2.     Matokeo ya uongo huo ni kutaka kuisaidia CCM na kugeuza mjadala.

3.     Idara ya Habari ya CHADEMA inapenda kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini kwamba,Mwenyekiti wa Chama Taifa, ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.

4.     Kwa uhakika tunapenda kuiambia jamii ya Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini, kwamba; Chama wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali popote na wakati wowote, hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa.

5.     Tungependa kuwaambia waliozusha tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza heshima kidogo waliyobakiza katika jamii kutokana na kuelemewa na mzigo wa tuhuma za utovu wa maadili na usaliti dhidi ya CHADEMA, badala ya kugeuka kuwa mabingwa wa kupika uongo, wajibu masuala ya msingi yanayowaandamana kuhusu mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na viongozi wake, ambayo iwapo chama kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu, ingesababisha kuua ndoto na matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani.

6.     Taarifa kuhusu baadhi ya tuhuma katika mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti wa Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli zake binafsi za uwekezaji, zitajibiwa kupitia taasisi husika.

Imetolewa leo Dar es Salaam na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

TAHADHARI YA UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA