Monday, 13 January 2014

NYOTA wa Madrid, Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia-2013( FIFA Ballon d'Or)

Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiwa amebeba tuzo yake ya uchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2013 kwenye halfa hiyo ya Fifa Ballon d'Or iliyofanyika jumatatu Zurich-Uswisi. Ni mara ya pili kwa mchezaji huyo wa Ureno kujinyakulia tuzo hiyo baada ya kushinda mwaka 2008 akiwa akiichezea timu ya Manchester United.
 

Cristiano Ronaldo akijipangusa machozi baada ya kupanda stejini kwa ajili ya kupokea tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2013. Akimpongeza ni nyota wa Zamani, Pele.
 

Cristiano Ronaldo na mwanae amabye pia anaitwa Cristiano aliyeongozana nae kupokea tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2013 katika halfa ya Fifa Ballon d'Or iliyofanyika Zurich-Uswisi.
Cristiano Ronaldo na mpenzi wake, Irina Shayk wakiwa kwenye tuzo ya ifa Ballon d'Or Zurich-Uswisi.
Lionel Messi na mkewe, Antonella.
Nyota wa zamani wa Brazil, Ronaldo Delima akiwa na mkewe kwenye tuzo za Fifa Ballon d'Or Zurich-Uswisi.

Zidane akimpongeza Franck Ribbery.

ZURICH , Uswisi - Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2013(FIFA Ballon d'Or), na kusimamisha mbio za Lionel Messi alieshinda tuzo hizo kama mchezaji bora wa dunia kwa miaka minne mfurulizo.

Ronaldo alifunga mabao 69 kwa Real Madrid na Ureno mwaka jana, na kufunga Hat-trick ya ajabu dhidi ya Sweden katika mchujo wa Kombe la Dunia zitakazo chezwa Brazil.

"Hakuna maneno yatakayoweza kueleza wasaa huu," alisema Ronaldo, ambaye alionekana akitokwa na machozi baada ya kupokea tuzo hiyo akiwa na mtoto wake mdogo, ambaye pia jina lake ni Cristiano.

Ronaldo amewashinda Messi(Barcelona) na winga wa Ufaransa(Franck Ribery), anayeichezea timu ya Bayern Munich.

Upigaji wa kura ili kupata mshindi ulifanyika na makapteni wa timu ya taifa, makocha, pamoja na baadhi ya waandishi wa habari walioteuliwa, katika nchi FIFA ya 209 wanachama ambao waliamua juu yao -3 upendeleo.

Kura hizo zilionesha Ronaldo kupokea pointi 1365 , huku Messi alikuwa na pointi 1205 na Ribery akipata pointi 1127.
Kocha wa Canada, Benito Floro alitupa kura yake ya kwanza kwa Ronaldo, wakati nahodha Atiba Hutchinson atupa kura yake ya kwanza kwa Messi na Ronaldo ya pili .

Ronaldo alionekana akifunga macho yake wakati nyota wazamani wakibrazil, Pele aliposoma jina lake huku akitabasamu.
Roanldo alimbusu mpenzi wake, Irina Shayk , kabla ya kupanda stejini kwa ajili yakupokea tuzo hiyo.

"Watu ambao wananijua wanafahamu watu wangapi wamenisaidia , " alisema mshindi huyo kwa hisia katika lugha ya kireno.
Akiongeza "Kama nimemsahau mtu yeyote naomba anisamehe."

Ronaldo alisubiri kwa mda wa miaka mitano tangu kushinda tuzo ya kwanza kama mchezaji bora wa dunia mwaka 2008 akiwa anachezea timu ya Manchester United, kwa kuwa Messi alikuwa akimpiku kwa miaka minne mfurulizo.

No comments:

Post a Comment