Paul Walker enzi za uhai wake. |
Paul Walker
alikutwa amekufa katika hali ya ukakamavu wakutaka kujiokoa dhidi ya mateso
ya ajali ile “Pugilistic Stance” na pia sehemu nyingi katika mwili wake zilikuwa zimevunjika ikiwemo taya,
mkono wa kushoto na mbavu, hii ni kulingana na ripoti ya Coroner iliyotolewa siku
ya Ijumaa.
Gari alilokuwa amepanda Paul Walker pamoja na Rodas. |
TMZ imeripoti kwamba Walker(40 ), alikutwa katika hali ya kutaka kujihami dhidi ya ajali ile kabla ya kukutwa na umauti siku ya Novemba 30. Ajali hiyo pia ilisababisha kifo cha dereva, Roger Rodas, rafiki na mfanyabishara mwenza wa Walker.
Kwa mujibu wa Medical Dictionary , “Pugilistic stance msimamo wa kujihami linalofananishwa na jinsi mabondia wanavyosimama wakijihami wakati wa pambano ambayo pia ni kawaida kuonekana katika miili ambayo imechomwa na moto , ikihusisha pia kupinda kwa kiwiko, magoti, hipsi na shingo, na kujifunga kwa nguvu kwa mkono wa ngumi , hii inasababishwa na joto kali katika moto , na kusababisha misuli kukakamaa, hutokea hata kama mtu alikuwa amekufa kabla ya moto”.
Ripoti wamesema kwamba mwili wa Walker ulmekutwa umeungua sana kiasi kwamba hamna kiungo chake atakimoja kinachoweza kuchangiwa kwa mgonjwa.
Walker na Rodas walikufa katika ajali Novemba 30 wakitokea Kusini mwa California.
Gari lilikuwa likisafiri
kwa "kasi isiyosalama" ya "takriban 100 + mph" kabla ya kupata
ajali.
Paul Walker na Vin Diesel katika moja ya scene ya movie inayokuja ya "Fats & furious 7". |
No comments:
Post a Comment