Saturday 28 December 2013

FAINALI YA SHINDANO LA 'MO KIDS GOT TALENT' LILIVYOFANA JANA LEDGER PLAZA BAHARI BEACH.

Mtoto Moureen Julius(12) amejinyakulia kitita cha shilingi milioni tano katika fainali za Shindano la 'MO KIDS GOT TALENT 2013' lililofanyika kwenye hoteli ya Ledger Plaza Bahari beach kuanzia tarehe 25 hadi jana tarehe 28 ambapo fainali zilifanyika.
Shindano hilo lilijumuisha watoto zaidi ya mia mbili ambapo kila mmoja alijipatia nafasi ya kuonesha kipaji chake vikiwemo kuogelea, kuimba, kucheza, karate n.k
Watoto 15 walichuana katika nusu fainali na kuchujwa hadi kufikia watoto watano na mwisho wa siku kupatikana SUPER STAR Moureen Julius aliyewafunika wenzake kwa kipaji alichonacho.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza aliyejinyakulia kitita cha sh.millioni tano, Mtoto Moureen Julius alisema pesa hizo alizoshinda atazitumia kwa kulipia ada na  vifaa vingine vya shule.
Shindano hili la 'MO KIDS GOT TALENT 2013' liliandaliwa na Frost Africa na kudhaminiwa na Mohammed Enterprises Tanzania Limited.

Huyu ni Salum akiimba 'Number One' ya Diamond Platnumz




Ni mwendo wa kuonesha vipaji tuu!!
Marapper hawakukosekana pia.
Moureen akionesha kipaji chake cha kucheza.
Mtu na dada yake nao walishirikiana kuimba wakiwania kitita kile cha sh.milioni tano.
Lisa akionesha kipaji chake cha kucheza. Hapo alikuwa anacheza song hit ya Davido 'Skelewu'
Peter wa Bongo movie 'Uncle JJ' naye alikwepo kuwapa support watoto wenzake.



Watoto hawakuwepo mbali kuwatazama na kuwapa support wenzao.
Mr. DJ full mzuka hapo. Ndiye aliyesimamia show mwanzo mwisho!
 

Waandishi wahabari nao walikwepo kushudia shindano hilo katika hoteli ya Ledger Plaza Bahari beach jana.



Top 5


Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Fatema Jaffer akizungumza katika shindano hilo, Pamoja naye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Peter Sekasiko, waandaji wa shindano hilo.
Dakika moja moja ilitolewa kwa kila aliyeingia Top 5 kwa ajili ya mchuano wa mwisho.
Top 5 wakisubiria kuchujwa mmoja baada ya mwingine. Hapo kiroho juu!
Mshindi wa tano akikabidhiwa zawadi yake.
Mshindi wa nne akikabidhiwa zawadi yake.
Salum akimfariji Moureen baada ya kubakia wawili kwenye shindano hilo.
Haya sasa mda umefika wa kumjua mshindi wetu. Raisi wa wanafunzi, Allan Lucky(kulia) akijiandaa kumtaja mshindi wa 'MO KIDS GOT TALENT'
Moureen akilia kwa furaha.
Moureen akikumbatiana na baba yake kwa furaha ya machozi.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Jaffer akimkabidhi Moureen Julius fesha taslim sh.milioni tano mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la 'MO KIDS GOT TALENT' jana katika hoteli ya bahari beach jijini Dar es Salaam.
Milionea Moureen akipozi na mtonyo wake.


No comments:

Post a Comment