Tigo
Tanzania imezindua mashine maalum ya pili ya TigoMatic inayowawezesha
wateja wake kulipia bili za huduma mbali mbali na kuongeza salio itakayofanya
kazi kwa masaa ishirini na nne kwa siku.
Uzinduzi
huo umehudhuriwa na Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, ambaye ameipongeza
Tigo kwa kuwa kampuni ya mawasiliano kwanza nchini Tanzania kuanzisha huduma ya
aina hiyo nchini.
“Ubunifu
huu wa Tigo si tu wa manufaa kwa wateja wake bali pia ni hatua mojawapo kubwa
ya kimaendeleo kwa nchi yetu katika matumizi ya teknolojia za mawasiliano za
kisasa duniani katika sekta ya mawasiliano,” alisema Dk Masaburi.
Dk
Masaburi alisema huduma mbalimbali zitolewazo na makampuni ya simu zikiwemo kupiga
simu, SMS, intaneti pamoja na huduma za kutuma na kupokea fedha zimeleta
mageuzi chnaya katika ufanyaji biashara na kuchangia kuboresha maisha ya
mamilioni ya watanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika katika tawi la huduma kwa wateja la Tigo
lililopo Masaki, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaeem Khan, amesema
uzinduzi wa ‘TigoMatic’ utawawezesha wateja wa Masaki kupata huduma za
zitolewazo na Tigo kwa masaa ishirini na nne kwa siku.
“Habari
njema kwa watu wa Masaki ni kwamba hakutakuwa na ulazima tena kwa wateja kukaa
kwenye foleni kwa ajili ya kupata huduma kutoka kwenye matawi yetu na sehemu nyinginezo
za mauzo kwa sababu mashine hii ya TigoMatic inatoa msaada wa mteja kujihudumia
mwenyewe,” alisema Bw. Khan.
Hii ni
mashine ya TigoMatic ya pili kuzinduliwa jijini Dar es Salaam na kampuni ya
simu Tigo. Mwezi uliopita Tigo ilikuwa kampuni ya simu ya kwanza nchini kuzindua
matumizi ya aina hii ya mashine ilipoanza kutoa huduma hii katika tawi la makao
makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Kijitonyama.
Akielezea
jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi, Bw. Khan alisema TigoMatic ni mashine
ambazo mteja anaweza akajihudumia yeye mwenyewe kama ilivyo kwa mashine za
kibenki za ATM ambapo mteja anaweza akafanya miamala tofauti tofauti bila
kuhitaji kuhudumiwa na mfanyakazi wa benki. Alisema kwamba wateja wa Tigo
hawatakuwa na ulazima wa kujisajili upya kwa ajili ya kutumia mashine hizo.
Khan
alisema kampuni inaazimia kuweka mashine zake katika matawi yake yote ya huduma
kwa wateja nchi nzima pamoja na sehemu za mikusanyiko mikubwa ya watu kama vile
maduka makubwa, stendi za mabasi, mitaani, viwanja vya michezo na
mahospitalini.
No comments:
Post a Comment