Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika. |
Mkutano huo wa Mbunge na wananchi utafanyika katika eneo la Luguruni Makondeko na utahusisha pia kamati ya waathirika wa hifadhi ya barabara pamoja na wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali ya majimbo ya Ubungo, Kisarawe na Kibaha.
Wananchi hao wamekuwa na malalamiko ya haki zao za msingi za makazi na za kibinadamu kuvunjwa kwa maagizo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli ambayo hutekelezwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) kinyume na sharia.
Aidha, kwa nyakati mbalimbali katika ya mwaka 2011,
2012 na 2013 yamejitokeza malumbano ndani na nje ya Bunge baina ya Mbunge
Mnyika (akiwakilisha wananchi) na Waziri Magufuli (akisisitiza msimamo wa serikali)
kuhusu utata wa upana wa barabara ya Morogoro na haki za wananchi wanaoishi
maeneo ya pembezoni ya barabara hiyo.
Kwa upande mwingine, Malalamiko hayo ya wananchi
yalishawahi kufikishwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia shauri Na
80 la 2005 na hukumu kutolewa tarehe 31 Mei 2013, ambapo Mahakama Kuu ilitamka
kuwa sheria ya The Highway Ordinance Cap 167 Government Notice No 161 of
5/5/1967 ambayo hutumiwa na Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuingia katika
ardhi za wananchi “ni batili kwa kutofautiana
na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”.Kamati ya waathirika wa hifadhi ya barabara imemwandikia barua mbunge kumweleza kuwa mahakama kuu imeamua kuwa inayodaiwa na walalamikiwa (Wizara ya Ujenzi) kuwa ni hifadhi ya barabara (hadi Mita 121 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro pande zote mbili), iligawiwa kwa walalamikaji kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi wakati wa operesheni vijiji ya miaka 1970, na hivyo kwa mujibu wa vifungu vilivyotajwa hapo juu ni mali halali ya wananchi.
Katika mkutano huo, mbunge atasikiliza malalamiko ya wananchi juu ya hatua ya Wizara ya Ujenzi na Tanroads bila kujali hukumu ya mahakama kuendelea kushikilia ardhi za wananchi zilizo nje ya mita 30 kutoka katikati ya barabara isivyo halali bila ya kulipa fidia stahili katika maeneo ambayo Serikali inataka kuyatwaa kwa ajili ya miundombinu na kuwazuia wananchi kuendeleza maeneo yao yaliyo nje ya mipango ya maendeleo ya umma.
Mbunge anakwenda kukutana na wananchi kwa kuzingatia
kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
lilitunga Sheria ya barabara namba 13 ya 2007, na Kanuni zake kupitishwa
kupitia Tangazo la Serikali namba 21 la tar 23 Januari 2009. Kifungu cha 29,
kinataja upana wa hifadhi za barabara kuu na za mikoa (Trunk and regional
roads) utakuwa ni mita 60 tu, ikihusisha mita 30 kila upande kutoka katikati ya
barabara”.
Aidha
kifungu 27 A cha Kanuni hizo kinataja upana wa njia za barabara za lami
(lanes), kwa barabara kuu (Trunk roads), kuwa hautakiwi kupungua Mita 3.25. Kwa
maana hiyo hifadhi ya barabara ya mita 60 inaweza kutumika kujenga njia
zinazohitajika.
Maana
yake ni kwamba Wizara ya Ujenzi na
Tanroads wanaweza kuheshimu maamuzi ya mahakama na sheria za nchi na kuwezesha
barabara ya Morogoro kujengwa na kupanuliwa kwa njia za kutosha huku ikiacha
eneo la ziada kwa ajili ya wananchi kuweza kujiendeleza na kuendeleza Jiji.
Hivyo,
mkutano huo wa mbunge na wananchi utatoa nafasi ya hatua kupendekezwa
zitakazowezesha kulindwa kwa haki za msingi za wananchi lakini pia kufanikisha
maendeleo ya nchi kwenye sekta muhimu za ujenzi wa makazi na miundombinu.
Imetolewa
tarehe 18 Januari 2014 na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo:
Aziz
Himbuka
Katibu
Msaidizi
No comments:
Post a Comment