JUMLA ya fedha taslimu shilingi milioni
160 zimezolewa na wateja wa Tigo mara baada ya kampuni hiyo ya simu kuchezesha droo yake ya
pili katika promosheni yake ya ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ iliyofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa droo hiyo Mratibu wa promosheni za
Tigo Pesa, Bi. Mary Rutta alisema kwamba wateja watano walijishindia milioni 10
kila mmoja, wateja wengine 20 wamejishindia shilingi milioni 20 kila mmoja na wengine
350 walijishindia shilingi laki mbili mbili.
Washindi wa tano wa zawadi nono ya shilingi milioni
10 ni Bi. Irene Francis Mushi (25) ambaye ni
mfanyabiashara wa vipodozi kutoka Moshi, Bi. Magadalena Daniel Asei (37) mfanyakazi wa
DHL mkazi wa Kigamboni-Dar es Salaam
na Bi. Hilda Laurence Nyambo (56) ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Bima kutoka Kinondoni, Dar es Salaam.
Wengineni
Bi. Maria JumaMbata (26) mhitimuwa Chuo Kikuu mkazi wa Iringa na Bw.
Aloyce Idrisa Njole (23) mwanafunzi wachuo cha ufundi anayetoka mkoani Morogoro.
“Tigo
inafuraha kubwa sana kwasababu imewezakuleta tabasamu katika nyuso za wateja wake
katika kipindi hiki cha mwaka mpya.
Tunaamini kwamba zawadi hizi zitawafurahisha na kuwa fanya washerehekee sikukuu hii ya kuuaga mwaka
2013 kuingia 2014 kwa namna yakipekee,” alisema Bi. Rutta.
Aliongeza,
“Kwa ujumla zawadi zilizo shindaniwa jana ni milioni 50
kwa washindi watano waliopatikana, milioni 40 kwa washindi 20 na milioni 70
kwa washindi 350 ambapo kila siku wateja 50 walikuwa wanajishindia shilingi laki 2
kila mmoja, iliyofanya jumla kuwa shilingi milioni 160.”
Kwa mujibu wa Mratibu huyo wa Promosheni droo hii ilikuwa ya kuanzia tarehe
24 hadi 30 Desemba.
Utaratibu washindano hili unaruhusu wateja waliosajiliwa na
Tigo Pesa kushiriki katika promosheni hii kwa kutuma fedha, kununua bidhaa kupitia Tigo
Pesa, kutoa fedha, kununua muda wa maongezi au kulipia huduma mbali mbali kupitia Tigo
Pesa. Promosheni hii itaisha Februari 12 mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment