Monday, 23 December 2013

UBUNGO HALI TETE, ABIRIA WAKWAMA USAFIRI, MSURURU WA KUKATA TIKETI HAUFAI

'TUNAENDA NYUMBANI KUHESABIWA'

Ongezeko la wasafiri waendao mikoani kwa ajili ya kusherekea sikukuu za krismas na mwaka mpya umepelekea idadi kubwa ya wasafiri kukwama kutokana na mabasi kuwa machache na kushindwa kukidhi idadi ya wasafiri kama ionekanavyo katika picha abiria hao wakiwa hawana mwelekeo wa mda gani na lini watakapo anza safari zao. Abiria hao wamekwama leo katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mama na mtoto wakiwa na nyuso za majonzi baada ya kusubiri usafiri kwa mda mrefu katika stendi kuu ya mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

Idadi kubwa ya abiria wakisubiria usafiri wa kwenda mikoani na wengine wakionekana kuwasiliana na ndugu zao kwa nia ya kuwa taarifu juu ya tatizo la usafiri leo katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Abiria wakiwa wamejipanga katika mstari wakisubiria kukata tiketi leo katika stendi kuu ya mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam ili kuelekea mikoani kusherekea sikukuu za krismas na mwaka mpya.
Baadhi ya wasafiri wa morogoro wakikata tiketi katika kampuni ya mabasi ya Abood leo asubuhi katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Msururu mrefu wa abiria, wengi wao wakiwa ni wasafiri wa mikoa ya morogoro, iringa, mbeya na tunduma.

2 comments:

  1. hatari sana........mstari kama wa kwenda kupiga kura bhana!

    But hili tatizo limekuwa likijirudia mara kwa mara, serikali ichukue hatua coz tatizo hili ni hatari kwa uchumi wa nchi.

    ReplyDelete
  2. Mstari ulikuwa mrefu sana na leo nilipita asubuhi hali bado ni ile ile. Hatua stahiki zinabidi zichukuliwe.

    ReplyDelete